Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba
NHC Bw. Nehemia Mchechu Kyando akizungumza na wageni waalikwa wakati wa
hafla ya uzinduzi wa uuzaji wa nyumba za mradi wa 711 uliopo Kawe jijini
Dar
es salaam, Nyumba hizi ziko kwenye majengo 7 yenye ghorofa 11 kila
moja ambayo yanatarajiwa kuchukua watu 1000 kwa na huu ni utangulizi
wa ujenzi wa mji mpya wa kisasa unaotarajiwa kujengwa eneo la Tanganyika
Pakers Kawe jijini Dar es salaam ambao ukikamilika utaweza kuchukua
watu 15000.
Watu wanaohitaji kununua nyumba
hizo wanatakiwa kufika ofisi za NHC Kinondoni au Makao Makuu ya Shirika
la Nyumba NHC Upanga au wanaweza kutembelea kwenye mtandao wa shirika
hilo kwa maelezo zaidi ili kununua nyumba hizo hafla ya uzinduzi wa
nyumba hizo ilifanyika mwishoni mwa wiki katika makao makuu ya shirika
hilo Upanga.
Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba
NHC Bw. Nehemia Mchechu Kyando akizungumza na wageni waalikwa wakati wa
hafla ya uzinduzi wa uuzaji wa nyumba za mradi wa 711 uliopo Kawe jijini
Dar es salaam. 
Meneja wa Masoko na Mauzo wa NHC,
Tuntufye Mwambusi akizungumza na Monica Joseph Mkurugenzi wa Kampuni ya
Monifinace Investment Group Limited wakati wa uzinduzi huo.
Meneja wa Masoko na Mauzo wa NHC,
Tuntufye Mwambusi akimsikiliza Bw. David Shambwe Mkurugenzi wa Fedha
Maendeleo ya Biashara NHC katika uzinduzi huo kulia ni Mwita Makenge
Mkurugenzi wa Kampuni ya Wegmar Limited na kushoto ni William Genya
Meneja Maendeleo ya Biashara NHC .
Meneja wa Masoko na Mauzo wa NHC,
Tuntufye Mwambusi akizungumza na kuelezea jinsi mradi huo utakavyokuwa
na mambo muhimu yaliyopo katika mradi huo huku akiwa na baadhi ya
wafanyakazi wa shirika hilo..
Baadhi ya wafanyakzi wakipozi kwa picha w.akati wa hafla hiyo
Meneja wa Masoko na Mauzo wa NHC, Tuntufye Mwambusi akifafanua jambo mbele ya waalikwa wakati alipokuwa akiuelezea mradi huo.
Baadhi ya wageni walikwa wakifuatilia maelezo mbalimbali kuhusu mradi wa 711 wa Kawe jijini Dar es salaam.
Meneja Masoko wa Shirika la Nyumba
la Taifa NHC Bw. Aden Kitomari akifafanua mambo mbalimbali wakati
akiuelezea mradi wa 711 uliopo Kawe jijini Dar es salaam.
Wageni waalikwa wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yakitolewa na maofisa mbalimbali wa shirika la Nyumba NHC.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
Nyumba NHC Bw. Nehemia Mchechu pamoja na wafanyakazi wa shirika hilo
wakifuatilia video zilizokuwa zikionyesha jinsi mradi huo utakavyokuwa
wakati wa uzinduzi uliofanyika Makao Mkuu wa shirika hilo Upanga.
Baadhi ya wageni waalikwa kutoa taasisi mbalimbali wakifuatilia uzinduzi huo.
Kutoka kulia ni Meneja wa Masoko
na Mauzo wa NHC, Tuntufye Mwambusi na Meneja Masoko wa NHC Bw. Aden
Kitomari wakimsikiliza Taji Liundi aliyekuwa MC wa uzinduzi huo.
Wageni mbalimbali walihudhuraia uzinduzi huo.


0 comments :
Post a Comment