“KUMBE DIAMOND NDIO SABABU YA CHEGE KUFANIKIWA KWENYE HILI”


@nkupamah blog


Msanii mkongwe anaefanya poa kwenye tasnia ya muziki nchini Chege Chigunda anataraji kuachia video yake mpya ya kimataifa inayo itwa Sweety Sweety ambayo itarushwa kwenye kituo cha MTV BASE nyimbo ambayo amewashirikisha wakali wanaosumbua Afrika kwa sasa Run Town wa Nigeria na Uhuru wa Afrika Kusini.IMG-20151217-WA0026
 Akizungumza na mtembezi.com Chege Chigunda ameshukuru msanii Diamond Platnumz  kwa kufanikisha kufanyika kwa hiyo video kwa kumuunganisha na baadhi ya wasanii wa Afrika Kusini, ili nyimbo hiyo iweze kutambulika  na kupigwa katika vituo vya ndani na nje ya nchi.IMG-20151217-WA0030
 Akizungumzia video hiyo Chege amesema ni video iliyoandaliwa na muongozaji mahiri Justin Campos ambapo wimbo upo katika mahadhi ya Afro Pop jambo ambalo anaamini itamfikisha mbali endapo itapata fursa ya kuungwa mkono na wadau wa muziki nchini.IMG-20151217-WA0031
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment