MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN ALIPOWASILI AFRIKA YA KUSINI KUHUDHURIA MKUTANO WA TANO WA WAKUU WA NCHI ZA AFRIKA NA CHINA.

SAM1 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Shulu Hassan, akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Afrika ya Kusini, Radhia Msuya, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa
Ndege wa Olver Tambo jijini Johannesburg jana Desemba 3, 2015 kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Tano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China. Picha na OMR
SAM2Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Shulu Hassan, akisalimiana Mwambata wa Kijeshi wa Tanzania nchini Afrika ya Kusini (Defence advisor) Brig. Gen Ibrahim A. Kimario, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Olver Tambo jijini Johanesburg jana Desemba 3, 2015 kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Tano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China. Katikati ni  Balozi wa Tanzania nchini Afrika ya Kusini, Radhia Msuya. Picha na OMR
SAM3Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Rais wa China, Xi Jinping, wakati wa Mkutano Mkuu wa Tano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China (China-Africa Forum) uliofanyika leo Dec 4, 2015 jijini Johannesburg. Mhe. Samia amemwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano huo. Picha na OMR
SAM5Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan (mwenye kitambaa cheupe)  akiwa kwenye Mkutano Mkuu wa Tano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China (China-Africa Forum) uliofanyika leo Dec 4, 2015 jijini Johannesburg. Mhe. Samia amemwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano huo. Picha na OMR
SAM6Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan (mwenye kitambaa cheupe katikati)  akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wakuu wa Nchi za Afrika baada ya ufunguzi wa Mkutano huo Mkuu wa Tano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China (China-Africa Forum) uliofanyika leo Dec 4, 2015 jijini Johannesburg. Mhe. Samia amemwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano huo. Picha na OMR
SAM7Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan (kulia) akiwa katika mazungumzo na Rais wa Msumbiji, Mhe. Filipe Jacinto Nyusi, walipokutana kwenye ufunguzi wa  Mkutano huo Mkuu wa Tano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China (China-Africa Forum) uliofanyika leo Dec 4, 2015 jijini Johannesburg. Mhe. Samia amemwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano huo. Picha na OMR
SAM8Baadhi ya washiriki katika Mkutano huo kutoka nchi mbalimbali za Afrika waliohudhuria ufunguzi wa mkutano huo leo jijini Johannesburg. Picha na OMR
SAM9Baadhi ya washiriki katika Mkutano huo kutoka nchi mbalimbali za Afrika waliohudhuria ufunguzi wa mkutano huo leo jijini Johannesburg. Picha na OMR
SAM10Baadhi ya washiriki katika Mkutano huo kutoka nchi mbalimbali za Afrika waliohudhuria ufunguzi wa mkutano huo leo jijini Johannesburg
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment