SANYA,China
Kwa mara nyingine tena, mrembo wa
Tanzania ameshindwa kunga’ara katika mashindano ya mrembo wa
Dunia.
Katika fainali zilizofanyika jana mrembo wa Tanzania, Lilian Kamazima,
hakuambulia chochote.
Mshindi wa Miss World 2015 ni binti
mwenye miaka 23 toka Hispania ,Mireia Lalaguna Royo. Nafasi ya pili
iliwenda kwa Mrusi , Sofia Nikitchuk wakati nafasi ya tatu ilikwenda
Indonesia ambayo iliwakilishwa na mrembo Maria Harfanti.
Siku mbili zilizopita zilisambaa taarifa
katika mitandao ya kijamii kwamba Lilian Kamazima amefika kumi bora,
lakini taarifa hizo si za kweli. kumi bora katika michuano hii
ilihusisha warembo toka mataifa ya Urusi,
Ufilipino, Guyana, Lebanon, Hispania, Afrika ya Kusini,Ufaransa, Australia , Jamaica na Indonesia.
Tangu mrembo Nancy Sumari aweke rekodi ya kuwa Miss World Africa, hakuna mrembo aliewahi kuifikia rekodi hiyo.
0 comments :
Post a Comment