NAIROBI,Kenya
Ndege moja ya abiria ya Air France
Boeing 777 AF463, inayohudumu kati ya Mauritius na Paris imelazimika
kutua kwa ghafla katika uwanja wa ndege wa kimataifa mjini Mombasa –
Kenya baada ya
kifaa kinachodhaniwa kuwa bomu kupatikana ndani ya choo
cha ndege hiyo.
Mhudumu mmoja wa ndege hiyo alimfahamisha rubani kuhusiana na kifaa hicho ndipo shughuli za kutua kwa dharura zikaanza.
Katika mtandao wake wa kijamii wa
Twitter, kamanda mkuu wa polisi nchini Kenya Jenerali Joseph Boinnet,
amesema kuwa ndege hiyo iliyokuwa njiani kuelekea Paris Ufaransa ikiwa
na abiria 473 na wahudumu 14 ilitua salama na abiria wote kuokolewa.
Ndege hiyo inasemekana kutua saa sita
usiku wa kuamkia leo Jumapili, huku wataalamu wa kutegua mabomu kutoka
jeshila wanamaji la Kenya wakiingia ndani ya ndege hiyo kukagua
kifurushi kilicholeta taharuki.
Habari za hivi punde zinasema kuwa maafisa wa upelelezi wanasemekana kuwa wamewatambua washukiwa wawili abiria wa ndege hiyo.
Shirika linalosimamia viwanja vya ndege
nchini Kenya linasema kuwa kifaa hicho kimeondolewa ndani ya ndege
hiyo.,Shughuli za kawaida za usafiri zimerejea
0 comments :
Post a Comment