Na Mwandishi Wetu
WAZIRIwa Habari,Utamaduni,
Michezo na Sanaa, Nape Nnauye anatarajia kumwakilisha Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwenye Tamasha la
Krismasi linalotarajia kufanyika Desemba 25 kwenye ukumbi wa Diamond
Jubilee jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa
Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama, Makamu huyo wa rais
alitarajiwa kuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo lakini kutokana na
majukumu mengine ya kikazi, hivyo tunaendelea na maandalizi ya tamasha
hilo.
Msama alisema wanamshukuru Nape
kukubali kuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo ambalo lina mlengo wa
kurudisha shukrani kwa Mungu baada ya uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba
25.
“Ni nafasi yetu kama Kampuni na
Watanzania kurudisha shukrani kwa Mungu baada ya kipindi ambacho
kilikuwa kigumu katika maendeleo ya Tanzania, alisema Msama.
Aidha Msama alitoa wito kwa
Watanzania kujitokeza kwa wingi kwenye tamasha hilo kwa sababu ya
kufikisha shukrani kwa Mungu baada ya uchaguzi Mkuu.
Alitaja viingilio kwa VIP ni
shilingi 50,000, viti maalum shilingi 10,000, viti vya kawaida shilingi
5000 na watoto shilingi 2000.
Msama aliwataja waimbaji
watakaopanda jukwaani siku hiyo ni pamoja na Rebecca Malope (Afrika
Kusini), Solomon Mukubwa, Sarah K, Faustin Munishi (Kenya), Rose
Muhando, Upendo Nkone, Jesca BM, Joshua Mlelwa, Kwaya ya Wakorintho
Wapili na KKKT Yombo.
“Maandalizi yamefanyika kwa kiasi
kikubwa yamefanyika, hivyo nawaomba Watanzania tujitokeze kwa wingi
siku hiyo ili kufanikisha asante kwa Mungu,” alisema Msama
0 comments :
Post a Comment