Shirikisho
la Mpira wa Miguu nchini (TFF) linatarajia kufanya mkutano wake Mkuu wa
Mwaka kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Regal Naivera jijini Tanga ambapo
wajumbe wa mkutano huo tayari walishatumiwa taarifa za mkutano.
Akiongea
na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa mikutano wa TFF,
Kaimu Mkurugenzi wa Sheria na Wachama, Elliud Mvela amesema maandalizi
ya mkutano huo yanaendelea vizuri.
Mvella amesema ajenda za mkutano
mkuu wa kawaida ni zile zilizopo kikatiba, ila itaongezeka ajenda ya
marekebisho ya katiba ambayo ni mapendekezo yaliyotolewa na FIFA.
Agenda za mkutano mkuu ni:
1.Kufungua Mkutano
2. Uhakiki wa Wajumbe
3. Kuthibitisha Ajenda.
4. Kuthibitisha Muhtsari wa Mkutano Mkuu uliopita.
5. Yatokanayo na Mkutano uliopita.
6. Hotuba ya Rais.
7. Ripoti kutoka kwa Wanachama
8. Kuthibitisha ripoti ya utekelezaji wa Kamati ya Utendaji.
9. Kuthibitisha ripoti ya Ukaguzi wa Hesabu 2013.
10. Kupitisha bajeti ya 2016
11. Marekebisho ya Katiba
12. Mengineyo
13. Kufunga Mkutano.
0 comments :
Post a Comment