Kikosi cha timu ya taifa ya
Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’ kinatarajiwa kuwasili kesho mchana
jijini Dar ess alaam kikitokea nchini Ethiopia kilipokuwa kinashiriki
michuano ya Kombe la Chalenji kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati.
Kilimanjaro Stars imetolewa katika
hatua ya robo fainali na wenyeji Ethiopia kwa mikwaju ya penati, baada
ya kutoka sare ya bao 1-1 katika dakika 90 za mchezo huo, na wenyeji
kushinda kwa penati 4-3.
Timu ya Kilimanjaro Stars
inayonolewa na kocha Abdallah Kibadeni na msaidizi wake Juma Mgunda,
iliongoza kundi lake katika hatua ya makundi kabla ya kukutana na
wenyeji Ethiopia katika mchezo wa robo fainali.
Katika michezo wa makundi,
Kilimanjaro iliibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Somalia, ushindi
wa mabao 2-1 dhidi ya Rwanda, na sare ya bao 1-1 dhidi ya Ethiopia.
Baada ya kurejea nyumbani, TFF kwa
kushirikiana na benchi la ufundi wataanza maandalizi ya michezo dhidi
ya Chad itakayochezwa Machi 2016 kuwania kufuzu kwa Fainali za Kombe la
Mataifa Afrika mwaka 2017.
0 comments :
Post a Comment