NAPE ALISHUKURU GAZETI LA MTANZANIA

@nkupamah blog On 01,december 2015

 Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Taifa Ndugu Nape Nnauye akisalimiana na Mhariri Mtendaji Mkuu wa kampuni ya New Habari (2006) LTD Ndugu Absalom Kibanda mara baada ya kuwasili kwenye ofisi za New Habari (2006) LTD Sinza, jijini Dar Es Salaam ambao wanatoa magazeti ya Mtanzania, Dimba, Bingwa na The African.
 Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Taifa Ndugu Nape Nnauye akizungumza kwenye kikao cha kutoa shukrani kwa kampuni ya New Habari (2006) LTD kwa ushirikiano mzuri walio uonyesha wakati wa kampeni za uchaguzi wengine pichani ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Umma CCM Makao Makuu,Ndugu Daniel Chongolo (kushoto) na Mhariri Mtendaji Mkuu wa kampuni ya New Habari (2006) LTD Ndugu Absalom Kibanda (katikati).
Mbunge wa Jimbo la Nzega mjini Ndugu Hussein Bashe (wa tatu kutoka kushoto) akichangia jambo wakati wa kikao cha Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mtama Ndugu Nape Nnauye pamoja na wahariri wa magazeti ya Mtanzania, Dimba, Bingwa na The African.

   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi  CCM Taifa, ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Mtama mkoani Lindi Ndugu Nape Nnauye leo amefanya ziara katika ofisi za New Habari (2006) LTD inayochapisha magazeti ya Mtanzania, Dimba, Bingwa na The African.

   Katika ziara hiyo Ndugu Nape alitoa salaam za shukrani kwa kampuni hiyo kwa ushirikiano mzuri walio uonyesha wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi oktoba 2015 na pia aliwaomba waendelee na ushirikiano huo huo katika kufanikisha utekelezaji wa yale ambayo CCM iliwaahidi wananchi pamoja na kumuunga mkono Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment