Tuesday, December 1, 2015
@nkupamah blog
Mkurugenzi wa elimu kwa mlipa kodi kutoka mamlaka ya mapato nchini TRA Richard Kayombo ametolea ufafanuzi juu ya kukamatwa kwa makontena 9 katika eneo la Mbezi Tank Bovu jijini Dar es Salaam ambapo mpaka sasa hivi Makontena hayo pamoja na madereva waliokuwa wanayasafirisha yako chini ya ulinzi mpaka wahusika watakapojitokeza.
Kayombo amesema kuwa makontena hayo yamenaswa usiku wa manane kwa msaada wa wasamaria wema waliotoa taarifa za kupakiwa kwa makontena hayo katika bandari kavu ya PMM.
Bwana Kayombo amesema TRA imetoa masaa 24 kwa mmiliki wa makontena hayo kujitokeza, vinginevyo watayafungua na kuyataifisha kama sheria inavyoelekeza
0 comments :
Post a Comment