Mhariri
Mtendaji wa New Habari Corporation Ltd, Absalom Kibanda akimkarbisha
Karibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye ambaye pia ni Mbunge wa
Mtama, alipotembelea Ofisi za kampini hiyo leo, Sinza jijini Dar es
Salaam
Karibu sana
Karibu sana hapa ni ofisini kwako
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisalimiana na Mhariri wa Habari wa gazeti la Mtanzania, Bakari Kimwanga
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa CCM, Godfrey Chongolo akisalimiana na Kibanda
Wakienda ukumbini
Wakiwa katika mazungumzo
Kimwanga akinukuu dondoo za mazungumzo
Khamis Mkotya akiuliza swali
Nape akijibu swali
Mazungumzo yakiendelea
Asha Bani akiandika dondoo za mazungumzo
Nape na Hussein Bashe wakifurahia jambo katika mazungumzo
Naam hayo ndivyo yalivyo…..
Mkurugenzi wa New Habari Corporation Erasto Matasya akizungumza
Mazungumzo baada ya mazungumzo
Nape akiwa na Absalom Kibanda na Asha Muhajj
Nape akiwa na Asha Bani
Nape akiagana na Bashe kabla ya kuondoka. Picha zote na Bashir Nkoromo
HABARI KAMILI
NA BASHIR NKOROMO
Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimesema, kitampa ushirikiano mkubwa, Rais Dk. John Magufuli, ili aweze kwa ufanisi zaidi mapambano yake dhidi ya mafisadi na mikakati mingine ya kuinua uchumi wa Watanzania.
NA BASHIR NKOROMO
Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimesema, kitampa ushirikiano mkubwa, Rais Dk. John Magufuli, ili aweze kwa ufanisi zaidi mapambano yake dhidi ya mafisadi na mikakati mingine ya kuinua uchumi wa Watanzania.
Kimesema, kitampa ushirikiano huo Rais Dk.
Magufuli, kwa sababu, aliyoanza kuyafanya na atakayoyafanya baadaye
katika uongozi wake wa Urais anatekeleza yale yaliyomo katika ilani ya
Uchaguzi ya CCM ya 2015-2020.
Hayo yalisemwa na Katibu wa NEC, Itikadi
na Uenezi, Nape Nnauye alipokuwa akijibu maswali kadhaa yaliyoulizwa na
baadhi ya wahariri, aliokuwa akizungumza nao, katika ziara aliyofanya leo, katika Kampuni ya New Habari Corporation, Sinza jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wahariri, waliohoji ni kwa nini
CCM haijitokezi kumpongeza Dk. Magufuli katika juhudi ambazo ameanza
kuonyesha katika kupambana na ufisadi ikiwemo kubana fedha za walipa
kodi ambazo zingepotea bure katika masuala yasiyo ya lazima na wakati
huohuo kuanza kuwabana wafanyabiashara wanaodaiwa kukwepa kulipa ushuru.
“Yapo mengi tuliyoanisha katika ilani yetu
ya Uchaguzi, na yote yahahusiana sana na haya mnayoyaona yanafanywa na
Rais Dk. John Magufuli, tena Ilani hii tumeitunga hata kabla ya kumteua
kugombea Urais, Sasa anachofaya ni kuitekeleza ilani hii, isipokuwa
mbinu anazotumia ni ubunifu wake na hili hatuna tatizo nalo kama Chama
maana kiongozi wa aina hii ndiye tuliyemtaka”, alisema Nape.
“Najua wapo wanaojaribu kutengeneza
magingira ya kumtaka kumtenganisha Dk. Magufuli na CCM, nawambieni Dk.
Magufuli ni zao la CCM na mwana CCM Kindakindaki, hivyo ni upotoshaji wa
hali ya juu kujaribu kuuaminisha umma kwamba anayofanya Dk. Magufuli
hayana uhusiano na maelekezo ya CCM”, aliongeza Nape.
Alisema, baada ya kutengeneza ilani yake,
CCM, ilidhamiria kwamba, awamu hii ya tano ni ya kutafsiri uchumi katika
nyanja za huduma za Jamii, ikiwemo miundomboni, maji, afya na elimu.
“Ni kutokana na lengo hili, ndiyo sababu
tukakaa kwa makini na kuhakikisha ilani hii ya sasa tunamkabidhi mwana
CCM ambaye utekelezaji wake hautakuwa wa mashaka mashaka, Ndiyo huyo Dk.
Magufuli, bila shaka sasa na ninyi ni mashahidi mmeanza kuuona
utekelezaji wake wa ilani”, alisema Nape.
Akizungumzia kuhusu Rais Dk. Magufuli
kuchelewa kutangaza Baraza lake la Mawaziri, Nape alisema, Chama Cha
Mapinduzi kimeshaunda serikali kwa kumpata Rais, kilichobaki sasa ni kwa
Rais mwenyewe kuteua watendaji wake, lakini katika kufanya hivyo hakuna
mda aliopangiwa kuanza kufanya hivyo na hashurutishwi na Chama wala
sheria.
Nape alisema, Dk. Magufuli hachelewi
kuteua Baraza la Mawaziri kwa sababu anakosa wakuwateua, isipokuwa,
anayo namna na mda ambao mwenyewe Kama Rais amejipangia, na mda huo
ukijiri wa kuamua kufanya hvyo atafanya.
“Tatizo hapa ni kwamba mnayo kiu kubwa ya
kutaka kujua nani atawateua, sasa kiu yenu imepita kiasi, ndiyo maana
mnaanza kuhoji, lakini mimi naamini Dk. Rais Magufuli ataikata kiu yetu,
wala msipate taabu ya kuhoji kila kukicha”, alisema Nape.
Nape alisema, mbali na Chama kutengeneza
ilani ambayo italeta mageuzi makubwa ya kiuchumi hapa nchini, pia
Watanzania watarajie kuona mageuzi makubwa ndani ya CCM, kwa sababu yapo
njiani kuwadia.
“Kama ilivyo kawaida yetu, kila baada ya
uchaguzi mkuu huwa tunafanya tathmini, baada ya tathmini hiyo, huwa
lazima tufanye mageuzi kwa yale ambayo tumebaini kuwa ni kikwazo kwa
uhai na maendeleo ya Chama katika nyanja mbalimbali, na mageuzi haya
tunayafanya kuzingatia mahitaji ya sasa na wakati ujao”, alisema Nape.
Kuhusu Mwenyekiti wa sasa Rais Mstaafu,
Jakaya Kikwete kumwachia Ueneyekiti Rais Dk. Magufuli, Nape alisema,
hayo si mambo mageni kwa CCM, imekuwa ikifanyika katika awamu zote za
Urais, hivyo Kikwete anaweza akaamua kumwachia kabla ya uchaguzi mkuu wa
CCM utakaofanyika mwaka 2017 au kabla ya hapo akiona inafaa.
Zanzibar
Akizungumzia mgogoro wa Zanzibar uliotokana na kufutwa uchaguzi mkuu wa Rais wa Zanzibar, Nape alikiri kamba ni mbaya na unaitia doa Tanzania, akisema, lakini akasisitiza kwamba njia pekee ya kuumaliza ni kwa mazungumza baina ya viongozi wa ndani bila kushirikishwa mataifa ya nje.
Akizungumzia mgogoro wa Zanzibar uliotokana na kufutwa uchaguzi mkuu wa Rais wa Zanzibar, Nape alikiri kamba ni mbaya na unaitia doa Tanzania, akisema, lakini akasisitiza kwamba njia pekee ya kuumaliza ni kwa mazungumza baina ya viongozi wa ndani bila kushirikishwa mataifa ya nje.
Alisema, msingi wa mgogoro uliojitokeza
Zanzibar, si wa kisheria, bali ni wa kisiasa zaidi, hivyo juhudi ziwekwe
kwenye mazungumzo kuutatua, na baada ya kuutatua yaendelee kufanyika
mazungumzo ambayo yataleta suluhisho la kudumu kwa kuwa imekuwa ni
kawaida kwa Zanzibar kuzuka migogoro kila baada ya uchaguzi mkuu jambo
linaloonyesha kuwa tatizo ni la asili zaidi kuliko inavyodhaniwa.
Katika mazungumzo yake na wahariri hao wa
New Habari Corporation Ltd, Wachapishaji wa magazeti ya Rais, Mtanzania
na Dimba, alivitaka vyombo vya habari nchini, sasa kushirikiana na
Serikali kulijenga taifa.
“Tunajua wakati wa kampeni kulikuwa na
mambo mbalimbali ambayo wakati mwingine vyombo vya habari vililazimika
kukampenia vinaowaona kuwa wanafaa kutokana na sababu mbalimbali, lakini
kama tulivyokuwa tukisema, kwamba baada ya uchaguzi maisha yataendelea,
sasa umefika wakati wa kuendelea na maisha tuwe kitu kimoja”, alisema
Nape.
Alivitaka vyombo vya habari, kusaidia
kuishari Serikali na CCM, katika kutekeleza yaliyo bora kwa taifa na
hata pale vyombo hivyo vitakapoona kwamba Chama au serikali vinaenda
kinyume, visihofii kukosoa.
Kwa upande wao, Mtariri Mtendaji wa Habari
Corporation, Absalom Kibanda akimpongeza Nape kwa ushirikiano ambao
amekuwa akivipa vyombo vya habari, na kumtaka aendelee kuwacha milango
wazi kwa waandishi wa habari kama ambavyo amekuwa akifanya.
Ziara hiyo ya Nape aliyoianza jana, kwenye
vyombo vya habari inatarajiwa kuendelea kesho kwa kutembelea vyombo
vingine vya habari vyenye makao yake makuu jijini Dar es Salaam.
0 comments :
Post a Comment