Nkupamah media
SHIRIKA la ndege la Etihad, ndege rasmi ya taifa kwa Falme za kiarabu limetangza
kuanzisha mipango ya kurusha ndege aina ya boeing 787s kwa safari za
kwenda Dusseldorf, Perth, Shanghai, Istanbul na Johannesburg kwa mwa
mwaka 2016.
Matarajio
ya kuwasili kwa ndege hizo mpya aina ya Boeing 787s ni ndani ya miezi
saba ijayo, kuanzia Mei 2016, ndege hizo “Dreamliners” zenye uwezo wa
kubeba abiria 299 zitaanza kutoa huduma kwenda Dusseldorf, Perth,
Shanghai, Istanbul na Johannesburg kutoka Abu Dhabi zikichukua nafasi ya
ndege zinazotumika sasa.
Kwa
sasa Shirika la ndege la Etihad lina ndege tano tu aina ya 787s ambazo
zinafanya safari zake kati ya Brisbane, Washington, Singapore na Zurich
moja kwa moja kutoka Abu Dhabi.
Matarajio
ya Shirika hilo ni kuongeza zaidi ya Boeing 66 ndani ya miaka kadhaa
ijayo ambapo ndege hizo aina ya “Dreamliners”zitakuwa ndege rasmi za
shirika hilo kwa masafa marefu.
James
Hogan, ambaye ni Rais na afisa mkuu wa shirika la ndege la Etihad
alisema: “Tangu kuanzishwa kwa ndege aina ya 787 ya kwanza katika huduma
za kibishara mnamo februari mwaka huu, tumekuwa tukipata maoni mazuri
kutoka kwa abiria wetu ambayo yamekuwa kama alama ya ubora wa hali ya
juu katika kanda na dunia nzima.
“Kuanzia
mwezi Mei mwakani, shirika la ndege la Etihad litazindua ndege mpya
Boeing 787 aina ya dreamliners zitakazotumika rasmi badala ya hizi
zilizopo kwa safari za masafa marefu ambapo zitatoa fursa kwa abiria
wetu kupanda ndege za teknolojia mpya.
“Abiria
na wateja wetu wa siku hizi wanapenda kusafiri bila kero wala pirika
pirika kwenye usafiri wa viwango vya juu, wanataka chaguo zuri zaidi na
bei nafuu. Hivi ndivyo vigezo vyao vikuu katika kuchagua na sisi hapa
Etihad tunajitahidi kufikia matarajio hayo kwa tafiti na uvumbuzi wa
aina mbalimbali kama vile kuleta ndege mpya na kuendelea kuboresha njia
zetu za usafiri.
Ndege
hizi mpya aina ya 787-S zitajumuisha ubunifu wa ndani ya kabini 28 za
“business studios” na siti 271 za “economy smart” zikiwa na utulivu,
burudani na uwezo wa kuunganishwa kwa mawasiliano zikiwa angani.
Upambaji
wa ndani na mwanga vimesukwa zaidi kwa ubunifu wa kiarabu zikiendana na
ubunifu mpya wa kutoka “Abu dhabi” ulioletwa na shirika la ndege hili
katika uzinduzi mpya mwaka jana.
Ratiba ya Boeing 787 kwenda DUSSELDORF, kuanzia Mei mosi 2016 (muda wa Abu Dhabi):
Ndege Na.
|
Inaanzia
|
Inaondoka
|
Itawasili
|
Muda wa kufika
|
Mizunguko
|
EY0023
|
Abu Dhabi (AUH)
|
02:15
|
Dusseldorf (DUS)
|
07:20
|
Kila siku
|
EY0024
|
Dusseldorf (DUS)
|
11:50
|
Abu Dhabi (AUH)
|
20:25
|
Kila siku
|
Ratiba ya Boeing 787 kwenda PERTH, kuanzia Juni Mosi 2016 (muda wa Abu Dhabi):
Ndege Na.
|
Inaanzia
|
Inaondoka
|
Itawasili
|
Muda wa kufika
|
Mizunguko
|
EY0486
|
Abu Dhabi (AUH)
|
22:25
|
Perth (PER)
|
13:50 siku inayofata
|
Kila siku
|
EY0487
|
Perth (PER)
|
15:40
|
Abu Dhabi (AUH)
|
23:10
|
Kila siku
|
Ratiba ya Boeing 787 kwenda SHANGHAI, kuanzia Agosti Mosi 2016 (muda wa Abu Dhabi):
Ndege Na.
|
Inaanzia
|
Inaondoka
|
Itawasili
|
Muda wa kufika
|
Mizunguko
|
EY0862
|
Abu Dhabi (AUH)
|
21:55
|
Shanghai (PVG)
|
11:10 siku inayofata
|
Kila siku
|
EY0867
|
Shanghai (PVG)
|
00:30
|
Abu Dhabi (AUH)
|
06:25
|
Kila siku
|
Ratiba ya Boeing 787 kwenda ISTANBUL, kuanzia Agosti 1 2016 (muda wa Abu dhabi):
Ndege Na.
|
Inaanzia
|
Inaondoka
|
Itawasili
|
Muda wa kufika
|
Mizunguko
|
EY0097
|
Abu Dhabi (AUH)
|
09:05
|
Istanbul (IST)
|
13:10
|
Kila siku
|
EY0096
|
Istanbul (IST)
|
14:25
|
Abu Dhabi (AUH)
|
20:00
|
Kila siku
|
Ratiba ya Boeing 787 kwenda JOHANNESBURG, kuanzia Novemba Mosi 2016 (muda wa Abu Dhabi):
Ndege Na.
|
Inaanzia
|
Inaondoka
|
Itawasili
|
Muda wa kufika
|
Mizunguko
|
EY0604
|
Abu Dhabi (AUH)
|
10:00
|
Johannesburg (JNB)
|
16:40
|
Kila siku
|
EY0603
|
Johannesburg (JNB)
|
19:40
|
Abu Dhabi (AUH)
|
06:00 next day
|
Kila siku
|


0 comments :
Post a Comment