Wafuasi
wa Kasisi Felician Nkwera chini ya kituo cha Huduma za Maombezi
wameandamana leo jijini Dar es Salaam kumwomba mwenyezi Mungu aendeldee
kuilinda amani ya nchi pamoja na kuombea amani iliyopo iendelee kudumu.
Pichani ni sehemu ya umati
walioandamana kutoke eneo la Tazara mpaka Ubungo jirani na River Side
wakifanya sala, mfululizo wakiwa wamebeba sanamu za bikira Maria,
sakramenti ya ekaristi takatifu na kufukiza ubani kama ilivyo utamaduni
wa kanisa katoliki lililomtenga kasisi huyo miaka mingi iliyopita.
Kwa mujibu wa taarifa uiliyotolewa
na viongozi wa kituo hicho, haya ni matembezi ya sala ya tisa katika
mfululizo wa matembezi ya sala ambayo huduma za maombezi zimekuwa
zikifanywa jijini Dar es Salaam, Mbeya na Sumbawanga tangua
ilipoanzishwa mwaka 1969.
‘Huduma za maombezi ni
utumemaalumwa sala za tiba: yaani uponyaji wa maradhi na kupunga pepo.
Hauna ubaguzi kwa misingi yoyote na ni zawadi kutoka kwa Mungu kwa
Watanzania na ulimwengu mzima’ Alisema Kasisi Nkwera.
0 comments :
Post a Comment