Mahmoud Ahmad Arusha
WALIOKUWA wafanyakazi wa
mahakama ya kimataifa ya mauaji ya kimbari ya Rwanda, UN –ICTR, ambayo
imemaliza muda wake wakuwepo nchini , wameishitaki mahakama hiyo kwenye
mahakama ya kazi wakidai kutolipwa stahiki zao.
Wafanyakazi hao wakizungumza
kwenye ofisi ya Idara ya kazi mkoa wa Arusha, wamesema wanaishitaki
mahakama hiyo kutokana na kutowalipwa stahiki zao ambazo zinahusisha
Likizo na nyongeza ya mishahara kulingana na mikataba yao.
Wafanyakazi hao wanaidai
mahakama hiyo jumla ya dola za kimarekani, 800,000, ambazo hawajalipwa
hadi leo ambapo mahakama hiyo ya Umoja wa mataifa ambayo imedumu kwa
kipindi cha miaka 21 ilifunguliwa mjini Arusha mwaka 1994 nayo imemaliza
kazi yake mwezi uliopita.
Wafanyakazi hao ambao
waliajiriwa na Mahakama hiyo mwaka 1998 walikuwa wakihudumia wafungwa na
mabusu wa mahakama hiyo iliyopo kwenye gereza kuu la Arusha .
Wamesema walipoaanza kudai na
kufuatilia stahiki zao ndipo walipopewa barua za
kuachishwa waliachishwa kazi Septemba 30 mwaka huu .
Wamesema mara baada ya kupewa
barua zao hawakutakiwa tena kufika ofisi za Mahakama hiyo zilizokuwa
jengo la mikutano ya kimataifa AICC na ndipo walipofika Idara ya Kazi
mkoa kwa ajili ya kufungua shauri la madai yao.
Ofisi hiyo ya Kazi iliandikia
mahakama hiyo barua ya kutaka kufahamu stahiki za wafanyakazi hao lakini
mahakama hiyo haikujibu mpaka leo.
Wafanyakazi hao wamewasiliana na
kituo cha haki za binadamu , LHRC, mjini Arusha ambapo kimewapatia
msaada wa sheria ili kudai stahiki zao.
Akizungumza Wakili wa kituo cha
haki za binadamu, Shirinde Ngalule, amesema Umoja wa mataifa una kinga
ya kutokushitakiwa katika taasisi yeyote ile ikiwemo mahakamani.
Lakini kwa mjibu wa mkataba wa
kuanzishwa kwa mahakama hiyo hapa nchini Mahakama hiyo inatakiwa
kuendesha shughuli zake kwa kuzingatia sheria za nchi husika zikiwemo
sheria ya mahusiano ya kazi.
Amesema kwa msingi huo mahakama
hiyo inapaswa kuheshimu sheria na haki za binadamu, badala ya
kwanyanyapaa waliokuwa watumishi wake kwa kisingizio cha cha kuwa na
kinga ya kutokushitakiwa.
Amesema mahakama hiyo imekiuka
taratibu katika kuwaachisha watumishi hao ambao taratibu hazikufuatwa
ikiwemo kupewa notisi na badakla yake walipewa barua ya kuachishwa kazi
kitendo ambacho ni kinyume na haki za binadamu.
Ameongeza kuwa chanzo ni pale walipoanza kudai mkataba wa kazi ndipo walipoaanza kufukuzwa mmoja mmoja
0 comments :
Post a Comment