Msajili
wa vyama vya siasa nchini, Jaji Francis Mutungi amejibu tamko la Baraza
la Vijana wa Chadema (Bavicha) waliodai kuwa watamfungulia mashtaka
endapo hatachukua hatua dhidi ya CCM ikiwa ni pamoja na kukifuta chama
hicho kwa kuonesha ujumbe wa chuki na ubaguzi katika sherehe za
Mapinduzi ya Zanzibar.
Akiongea
na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Jaji Mutungi alisema
kuwa hawezi kuwazuia Bavicha kumpeleka mahakamani kwani hiyo ni haki
yao. Lakini akawashauri kuwa kabla hawajazungumza walichozungumza ni
vyema kwanza wangemuuliza na kuwa na uhakika kwani tayari ameshachukua
hatua za kisheria dhidi ya CCM.
“Wanatakiwa kuwa na uhakika kwanza,” alisema Jaji Mutungi. “Mimi
nimeshawachukulia hatua CCM, tena hatua kwa mujibu wa sheria.
Nimewaandikia barua nikiwataka wajieleze kuhusu ujumbe huo wa kibaguzi
ulioonekana,” aliongeza.
Katika
hatua nyingine, Jaji Mutungi alisema kuwa tayari ofisi yake
imeshaingilia mgogoro wa uchaguzi unaoendelea visiwani Zanzibar kwa kuwa
unawahusu wadau ambao ni vyama vya siasa.
Alisema amezungumza na pande mbili zinazozozana ili kusaidia katika kupata maridhiano ya amani.


0 comments :
Post a Comment