Rais
Magufuli amesema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa
Israel hapa nchini mwenye makazi yake Mjini Nairobi - Kenya Mheshimiwa
Yahel Vilan, Ikulu Jijini Dar es salaam.
"Natambua
mahusiano mazuri yaliyopo kati ya Tanzania na Israel, mahusiano haya ni
muhimu sana kwa ustawi wa nchi zetu mbili, nataka mahusiano haya
yaimarishwe zaidi " Alisema Dkt. Magufuli.
Aidha, Rais Magufuli ameahidi kuwa Tanzania itahakikisha inaanzisha ubalozi wake nchini Israel haraka iwezekanavyo.
Kwa
upande wake Balozi wa Israel hapa nchini Mheshimiwa Yahel Vilan pamoja
na kumpongeza Rais Magufuli kwa kazi kubwa na nzuri iliyofanywa na
uongozi wake katika kipindi kifupi cha miezi miwili tangu aingie
madarakani amemhakikishia kuwa Israel itaendelea kushirikiana na
Tanzania na ipo tayari kuimarisha zaidi mahusiano.
Balozi
Vilan ametaja baadhi ya maeneo ya ushirikiano katika uchumi kuwa ni
pamoja na Kilimo, Maji, Ufugaji wa Nyuki na Sayansi na Teknolojia huku
akibainisha kuwa Israel imewaalika Jumuiya ya wafanyabiashara wa
Tanzania kushiriki katika Kongamano la biashara kati ya Tanzania na
Israel litakalofanyika Mjini Tel Aviv nchini Israel, mwezi Septemba
mwaka huu.
Balozi
Vilan pia ameahidi kufikisha ujumbe wa Rais Magufuli kwa Waziri Mkuu wa
Israel Mheshimiwa Benjamin Netanyahu na pia ameahidi kuanzisha ofisi ya
kutoa huduma ya visa hapa nchini haraka iwezekanavyo.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU.
Dar es salaam.
19 Januari, 2016
Rais
wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifanya
mazungumzo na Balozi Yahel Vilan wa Israel hapa nchini Ikulu Jijini Dar
es salaam Januari 19, 2016
Rais
wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na
Balozi Yahel Vilan wa Israel hapa nchini Ikulu Jijini Dar es salaam
Januari 19, 2016 baada ya kufanya naye mazungumzo

0 comments :
Post a Comment