Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya
akizungumza na waandishi wa habari kuhusu watumishi wa wizara hiyo
nchini kote kupokea misaada inayotolewa na taasisi mbalimbali na watu
wenye moyo wa kusaidia jamii bila kujali itikadi za siasa au dini
isipokuwa wahakikishe misaada hiyo inakidhi viwango vinavyotakiwa.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya
akikabidhiwa nyaaraka muhimu na aliyekuwa katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dk
Donan Mmbando.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
Na Magreth Kinabo –Maelezo
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya
amesema misaada inayotolewa na watu mbalimbali kwa ajili ya kusaidia
jamii ni lazima iwe imekidhi viwango vya ubora, hivyo haitakiwi
kuangaliwa kwa vigezo vya dini, itikadi wala siasa.
Kauli hiyo imetolewa leo na
Katibu huyo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisi kwake baada
kituo kimojwapo nchini kukataa misaada iliyotolewa na Mbunge wa Bukoba
Mjini (Chadema), Wilfred Lwakatare wa Chama cha Wananchi(CUF), hivi
karibuni.
Dkt. Ulisubisya alisema hivi
karibuni gazeti moja la kila siku la hapa nchini liliripoti kwamba
misaada iliyotolewa na Mbunge huyo, katika baadhi vituo afya Zahanati
kwa ajili ya wajawazito kukataliwa.
“Serikali ina sera ya kusaidia
jamii hususan misaada inayotolewa kwenye huduma za afya, ambayo
inakidhi viwango vya ubora kulingana Sheria , kanuni na taratibu za
Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA),” alisema Katibu Mkuu huyo.
Kwa mujibu wa chanzo kimoja cha
habari kiliripoti kwamba baadhi ya wakuu wa vituo vya afya na zahanati
katika Manispaa ya Bukoba, wamegoma kupokea misaada kwa ajili ya
wajawazito uliotolewa na kwa madai ya kupewa maelekezo na Serikali.
Dkt. Ulisubisya aliwataka watendaji wa afya wa vituo hivyo
kuwa wasiangalie misaada hiyo kwa misingi ya dini, itikadi na kisiasa.
Hata hivyo Katibu Mkuu huyo aliwataka watu mbalimbali wenye lengo la kutoa misaada katika vituo vya afya kuhakikisha kwamba imekidhi viwango viliyowekwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA).
Hata hivyo Katibu Mkuu huyo aliwataka watu mbalimbali wenye lengo la kutoa misaada katika vituo vya afya kuhakikisha kwamba imekidhi viwango viliyowekwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA).
Katika hatua nyingine aliyekuwa Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dkt. Donan Mmbando alikabidhi ofisi hiyo kwa Katibu Mkuu huyo mpya


0 comments :
Post a Comment