Na RFI
Kundi la
Islamic State (IS) limeitishia Uingereza katika video mpya inayoonyesha
mauaji ya raia watano ambao kundi hilo limewaita "wapelelezi".
Video
hii, iliorushwa hewani Jumapili hii kwenye mitandao ya makundi ya
kiislamu na kuripotiwa na kituo cha
Marekani kinachofuatilia mitandao ya
makundi hayo, inaanza na "kukiri" mbele ya kamera kwa watu wanaodai
kuwa ni wakazi wa Raqa, "mji mkuu" wa kundi la Islamic state, nchini
Syria.
Watu hao wameonyeshwa na kundi hili la kigaidi kama "wapelelezi".
Kauli za
watu hawa watano hazionyeshi taifa au mataifa ambayo wanatuhumiwa
kufanyia upelelezi, lakini mmoja wao ameutaja muungano wa kimataifa
unaoongozwa na Marekani, ambao unaendesha vita dhidi ya kundi la Islamic
State katika nchi za Iraq na Syria.
Watu hao
wanasema kuwa wamekua wakipiga picha au video zinazoonyesha hali ya
maisha mjini Raqa kwa niaba ya watu wanaopiga kambi nchini Uturuki, au
pia kuchunguza harakati za wapiganaji wa IS.
Katika
video nyingine inaonyesha watu hao watano wakiwa wamevaa nguo za rangi
ya ya machungwa wanaovaa wafungwa wa IS, wakipiga magoti mbele ya watu
watano wanaoficha nyuso zao, ambao wote wamevaa sare za jeshi, huku
wakishikilia bastola.
"Huu ni
ujumbe kwa David Cameron, Waziri Mkuu wa Uingereza", mmoja wa wanamgambo
hao wa IS anasema kwa Kiingereza: "Ni jambo la kushangaza kusikia leo
kiongozi asioeleweka kama wewe anapinga nguvu za Islamic State".
Uingereza,
ambayo imekua ikiendesha mashambulizi dhidi ya ngome za IS nchini Iraq,
inaendesha tangu mapema mwezi Desemba mashambulizi ya anga nchini
Syria.
"Tutaendelea
na jihadi, tuvuke mipaka, na siku moja tutavamia nchi yako, ambapo
tutawala kwa mujibu wa Sheria za Kiislamu", mwanamgambo wa IS ameongeza.
"Kwa wale
ambao wanataka kuendelea kupambana chini ya mwelekeo wa Cameron, (...):
unawaza kweli kwamba serikali yako itakukumbuka wakati utakua umeanguka
mikononi mwetu? Au watakutupilia kama walivyowatupilia wapelelezi hawa
na wale waliokuja kabla yao? ", mwanamgambo wa Is amesema, akiwachagua
watu watano kupiga magoti mbele yake.
Mwishoni mwa hotuba yake, watu hao watano wameuawa kwa kupigwa risasi kichwani.(P.T)


0 comments :
Post a Comment