Trump ameendelea kusisitiza kwamba Waislamu wanafaa kuzuiwa kuingia Marekani
Mgombea
wa urais Marekani Donald Trump kwa mara nyingine ametetea pendekezo lake
la kutaka Waislamu wazuiwe kuingia Marekani baada ya wito huo kutumiwa
na wapiganaji wa al-Shabab kwenye
kanda ya video ya kutafuta wafuasi.
Bw Trump,
anayeongoza miongoni mwa wanaotafuta tiketi ya chama cha Republican,
amesema watu wamemsifu kwa kuwa na ujasiri wa kuangazia jambo hilo
“ambalo wengine wameamua kupuuza”.
Al-Shabaab
walitumia maneno hayo ya Trump kwenye video ya propaganda ya kutafuta
wafuasi wakisema ubaguzi wa rangi, ukatili wa polisi na chuki dhidi ya
Waislamu vimesheheni Marekani.
"Sasa watu wanaanza kuzungumzia hili,” ameambia kituo cha runinga cha CBS News.
Kundi
hilo liliweka sehemu ya kanda ya video ya Trump akikariri wito wake
wakati wa mkutano wa kampeni kwenye video yao ya propaganda ya karibu
saa nzima.
Katika
mahojiano na watangazaji wa kipindi cha Face the Nation cha CBS News,
ambacho kitapeperushwa baadaye Jumapili, Bw Trump aliulizwa kuhusu jinsi
al-Shabab wanatumia matamshi yake kutafuta wafuasi.
Trump yuko buheri wa afya, daktari asemaUS: Maneno ya Trump ni hatari kwa usalama
"Tazama,
kuna shida hapa. Nimeibua hili. Watu wengine wamenipigia simu na kusema
nina ujasiri kwamba niliibua hili kwa sababu ni ukweli mtupu na hakuna
anayetaka kuhusika.
"Watu ambao wameshawishika vingine na sasa wanasema, unajua, labda Trump hajakosea. Tunafaa kuangalia hili kwa kina zaidi.”
Bw Trump
alipendekeza Waislamu wazuiwe kuingia Marekani baada ya wanandoa
Waislamu kushambulia sherehe mjini San Bernardino, California na kuua
watu 14.
Wito wake ulishutumiwa snaa na viongozi mbalimbali duniani.
Matamshi ya Trump yalishutumiwa sana
Mgombea
urais wa chama cha Democratic Hillary Clinton alisema maneno ya Bw Trump
yanamfanya kuwa “mwandikishaji bora sana wa wanachama” wa kundi
linalojiita Islamic State.
Miaka ya hivi karibuni, Wasomali-Wamarekani kutoka Minnesota wameripotiwa kwenda Somalia kujiunga na al-Shabab.
Wapiganaji
wa al-Shabab, hutaka kuondoa madarakani serikali ya Somalia inayoungwa
mkono na mataifa ya Magharibi na kuweka utawala mkali wa Sharia.
Wametekeleza mashambulio ya kigaidi Kenya, Uganda na Ethiopia.BBC


0 comments :
Post a Comment