WATAALAM WATEMBELEA VYANZO VYA MAJI YA MABWAWA YA KUZALISHA UMEME

 VY1
Wataalam kutoka Wizara za Nishati na Madini,Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi ,Wizara ya maji, na Umwagiliaji , Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco )pamoja na Watalamu wa bonde la mto Rufiji walitembelea  vyanzo vya maji vinavyotiririsha  maji katika mito mikubwa inayomwaga maji
katika  mabwawa ya kuzalisha umeme wa maji ya  Mtera, Kihansi na Kidatu ili kuangalia uharibifu wa vyanzo hivyo vya maji na kuchukua hatua za kuzuia uharibifu huo
Wataalam hao waliunganisha nguvu ya pamoja ili kurejesha utunzaji na usalama wa  vyanzo hivyo  ili viwe katika hali yake ya awali kutokana na kuathiriwa na shughuli za kibinadamu zinazoendelea na kusababisha kukauka kwa maji na kusababisha upungufu mkubwa katika mabwawa ya kuzalisha umeme tofauti na  ilivyokuwa katika miaka ya nyuma.

Muonekano wa Bwawa la Kihansi kwa sasa ambalo pia limepunguza uzalishaji wa umeme wa maji kutokana na kupungua kwa kina cha maji.
VY2
Timu ya wataalamu  kutoka Wizara ya Nishati na Madini,Wizara ya kilimo, mifugo na uvuvi ,Wizara ya maji, na umwagiliaji , Shirika l Umeme Tanzania (Tanesco )pamoja na Watalamu wa bonde la mto Rufiji waliotembelea  vyanzo vya maji vinavyotiririsha  maji katika Mabwawa ya kuzalisha umeme wakiendelea na ukaguzi wao .
VY3
Eneo lenye  chanzo cha cha maji pamoja cha mto  Mbalo mto huu  hutumiwa kwa shughuli za kibinadamu na kusababisha upotevu wa maji yanayoingia katika  katika mabwawa ya kuzalisha umeme wa maji
VY4
Moja ya sehemu ya mashine ama mtambo inayotumika kuzalisha umeme wa maji katika vituo vya Kihansi, Kitadu na Mtera.
VY5
Mashine inayotumika kuondoa  taka  kama vile magogo na nyingine za
namna hiyo katika mabwawa ya kuzalisha umeme wa maji.
22709f7d-3f87-4d0f-b925-e712ddfa6542
Baadhi ya wajumbe wa Timu ya kutoka Wizara ya Nishati na Madini,Wizara ya kilimo, mifugo na uvuvi ,Wizara ya maji, na umwagiliaji , Shirika l Umeme Tanzania (Tanesco )pamoja na Watalamu wa bonde la mto Rufiji wakipata maelezo ya namna ambavyo umeme wa maji huzalishwa katika kituo cha Kihansi .
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment