WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amewapongeza Makatibu Wakuu na Naibu Katibu Wakuu,
mara baada ya kuapishwa Ikulu leo jijini Dar es Salaam.
Ametoa pongezi hizo wakati
Makatibu Wakuu na Naibu Katibu Wakuu wakiwa wametia saini hati
ya ahadi
ya uadilifu kwa viongozi wa umma mbele ya waandishi wa habari.
Waziri Mkuu Majaliwa pia amewataka
viongozi hao, kuwa waaminifu, kuwajibika na kutoa taarifa ya utendaji
kwa wananchi. Aidha, alisema kuwa, viongozi wengine watakao apa mbele ya
Kamishna wa Tume ya Maadili ni pamoja na Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa
Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri, ikiwa ni hatua ya Serikali
kudhibiti na kufuatilia matumizi ya rasilimali fedha.
“Wakuu wa Wilaya watahakikisha
fedha zilizoenda katika Halmashauri zao lazima zitumike katika shughuli
zilizokusudiwa” alisema Waziri Mkuu.
Waziri Mkuu alitoa wito kwa
watanzania kuendelea kuwa na imani na Serikali ya Awamu ya Tano, kwakuwa
itatimiza ahadi zote ambazo Mheshimiwa Rais na Makamu wa Rais walizitoa
wakati wa Kampeni.
Makatibu Wakuu na Naibu Katibu
Wakuu hao, wameapishwa na Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli, ambapo
shughuli hiyo ilihudhuriwa pia na Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia
Suluhu, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, Mke wa Mheshimiwa Rais
mama Janeth Magufuli pamoja na viongozi mbalimbali.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI
S.L.P 3021
1141O DAR ES SALAAM
IJUMAA, JANUARI 1, 2016.
0 comments :
Post a Comment