Nkupamah media:
Francis Cheka
Pambano hilo la uzito wa kati linalotambuliwa na Shirikisho la
Ngumi Duniani (WBF), lilifanyika usiku wa kuamkia jana jijini Dar es
Salaam.
Majaji watatu Anthony Lutta, Sako Mtulya na Ibrahim Kamwe wote
kutoka Tanzania, walimpa ushindi Cheka wa pointi 115-112, 115-112 na
116-111.
Baada ya pambano Cheka alisema kuwa ushindi wake haukuwa rahisi kwa vile mpinzani wake alikuwa mkali na kutumia nguvu nyingi.
"Ajetovic alitamba angenipiga kwa KO, lakini ilikuwa ngumu kwangu kutokana na kujiandaa vizuri," alisema Cheka.
Lakini mambo yalikuwa tofauti kwa mpinzani wake, Ajetovic aliyegoma
kuzungumza na waandishi wa habari akidai majaji 'walimpa' ushindi
Cheka.
Katika mapambano ya utangulizi Cosmas Cheka alimpiga Mustapha Dotto
kwa pointi na kufanikiwa kutwaa ubingwa wa WBF Afrika, huku Mohamed
Matumla akimdunda Bakari Mohamed na Seleman Zugo akimshinda kwa pointi
Mwinyi Mzengela na Mwanne Haji alimdunda Lulu Kayage katika pambano la
mabondia wanawake.
Abdallah Pazi alimpiga kwa KO raundi ya nne Baraka Mwansope, huku
Mohamed Amir akimshindilia makonde Yusuph Kombo na kuibuka mshindi kwa
pointi.
0 comments :
Post a Comment