Nkupamah media:
Jerry Muro, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga.
Katika miaka ya karibuni, timu hiyo ya Jangwani imeachana na
utaratibu wake wa kupiga kambi Bagamoyo mkoani Pwani kabla ya kucheza
mechi kubwa na badala yake imekuwa ikijichimbia visiwani Zanzibar.
Katika kile kinachoonekana kambi ya Pemba inalipa, mabingwa hao
mara 25 wa Tanzania Bara, wamefanikiwa kufunga mabao 4-0 katika mechi
mbili zilizopita dhidi ya watani wao wa jadi, Simba.
Na ili kufanya vyema Jumamosi dhidi ya wapinzani wao wakubwa kwenye
mbio za ubingwa msimu huu, Azam FC, kikosi cha Mdachi Hans van der
Pluijm kiliondoka jijini Dar es Salaam jana mchana kwenda Pemba kikipaa
kwa 'pipa' la kukodi.
Kwa mujibu wa Jerry Muro, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya
Yanga, nyota 23 na watendaji wengine wote wa benchi lao la ufundi
walikwea pipa jana kwenda Pemba kusaka dozi ya Wanalambalamba.
"Tumeamua kwenda na wachezaji wote 24, lakini waliosafiri leo
(jana) ni 23, (Donald) Ngoma bado hajarejea nchini (kutoka kwao
Zimbabwe)," Muro alisema.
"Tunatarajia atarejea nchini leo (jana) mchana au kesho (leo).
Pemba kuna utulivu na uwanja wa kapeti kwa ajili ya mazoezi. Ndiyo maana
tunapapenda kwa kambi za timu yetu."
Yanga wanaongoza msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara wakiwa na mtaji
wa pointi 46 baada ya mechi 19 sawa na Azam FC, lakini mabingwa watetezi
wapo kileleni kwa wastani mzuri wa mabao.
Mechi ya Jumamosi inatarajiwa kutoa taswira halisi ya timu itakayokuwa na nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa wa msimu huu.
0 comments :
Post a Comment