Nkupamah Media:
Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na
Kimataifa, Mhe. Dkt. Susan Kolimba (Mb) akiukaribisha ujumbe wa wabunge
wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje ya Bunge la Sweden walipomtembelea
leo ofisini kwake.Wabunge hao wapo nchini kwa madhumuni ya kutathmini na
kukagua miradi inayofadhiliwa na Serikali ya Sweden kwa Tanzania ili
kubaini utaratibu bora zaidi wa kusaidia Tanzania katika kipindi
kijacho.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na
Kimataifa, Mhe. Dkt. Susan Kolimba (Mb) (kulia) akizungumza na kiongozi
wa ujumbe huo, Mhe. Kenneth G. Forslund anbaye ni Mwenyekiti wa Kamati
ya Bunge ya Mambo ya Nje ya Sweden. Katika mazungumzo hayo, Dkt. Kolimba
alishukuru Serikali ya Sweden kwa misaada yake katika sekta ya elimu ya
juu na Bajeti ya Maendeleo. Aidha, Mhe. Naibu Waziri alisisitiza
umuhimu wa kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Sweden hususan
katika masuala ya kiuchumi na biashara.
Maafisa
kutoka Wizara ya Mambo ya Nje wakifuatilia mazungumzo hayo. Kutoka
kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Balozi Joseph
Sokoine, Bi. Tunsume Mwangolombe, Bw. Adam Issara na Bw. Ally Kondo.
Baadhi ya Waheshimiwa. Wabunge kutoka Sweden wakifuatilia mazungumzo hayo.
Sehemu nyingine ya Waheshimiwa Wabunge kutoka Sweden.
Naibu
Waziri, Dkt. Kolimba wa pili kutoka kulia akiwa katika picha ya pamoja
na wabunge wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje ya Bunge la Sweden.


0 comments :
Post a Comment