Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Charles Kitwanga (pichani) amewataka
Watanzania kuzingatia sheria za mtandao ambazo zilitungwa mwaka jana
kufuatia kuonekana kuwepo kwa baadhi ya watumiaji ambao wamekuwa
hawafati sheria.
Mhe.
Kitwanga alisema wanaotumia mtandao wanawajibu wa kutumia mtandao kwa
matumizi
ambayo hayatavunja sheria na ambao watakuwa wakikiuka sheria
hiyo serikali haitawavumilia na watawachukulia hatua za kisheria.
Msemaji wa Jeshi la Polisi Advera John Bulimba.
“Adhabu ya kuvunja sheria hii ya makosa ya mtandao ni mbaya sana na
ninataka kuwambia Watanzania wazingatie sheria za mtandao … kifungo ni
miaka 30 au hata zaidi,” alisema Kitwanga.
Aidha
aliwataka ambao wamekuwa wakitukanwa katika mitandao ya kijamii
wapeleke malalamiko Polisi na serikali imejipanga kuwachukulia hatua
watumiaji ambao wamekuwa hawafati sheria za mtandao.
Kwa
upande wa Jeshi la Polisi kupitia kwa msemaji wa jeshi hilo, Advera
Bulimba alisema kuwa jeshi hilo limekuwa likiwachukulia hatua watumiaji
wote wa mitandao ambao wamekuwa wakikutwa na hatia ya kufanya matumizi
mabaya.
Alisema
tangu imetungwa sheria hiyo wameshafungwa baadhi ya watumiaji na kesi
saba zikiwa mahakamani na bado wanaendelea kufatilia watumiaji wengine
ili wawachukulie hatua.
“Polisi
tunaendelea kuwachukulia hatua watumiaji ambao wanakuwa na makosa na
kwasasa kuna kesi saba zipo mahakamani … tangu sheria imetungwa kesi
tunazopokea zinazohusu mitandao zimepungua kutoka 25 hadi 30 kwa siku
ila siku hizi zinakuwa 10 au chini ya hapo,” alisema Bulinda.
Nae
mmoja wa watumiaji wa mtandao, Grace Mwanga aliwashauri Watanzania
wenzake kudumisha maadili ya kitanzania na kuifanya mitandao kama njia
ya mawasiliano kama jinsi lilivyo kusudiwa na waanzilishi wa mitandao
hiyo.
“Watanzania
tudumishe maadili yetu ya zamani, mitandao isitufanye tusahau asili
yetu … tutumie mitandao kuwasiliana na hata kufanya matangazo ya
biashara zetu,” alisema Grace.


0 comments :
Post a Comment