Mshauri wa masuala ya Elimu
kutoka Taasisi ya Aryan International Education Consultants ya nchini
China Dkt. Safdar Khattak akitoa maelezo kuhusu namna ya kujiunga na
Elimu ya Juu kwa wanafunzi wakitanzania waliotembela maonyesho ya
Kimataifa ya Elimu “Tanzania Internation Education Fair 2016”
yanayoendelea katika ukumbi wa British Council jijini Dar es Salaam
.
Mmoja wa wadau wa elimu aakijaza fomu ya kujiunga na Chuo Kikuu cha BPP cha nchini Uingeraza alipotembelea maonyesho ya Tanzania Internation Education Fair 2016 jana
jijini Dar es Salaam.Wanaomshuhudia ni Afisa Mtendajji Mkuu wa Taasisi
ya WR Education Placement Consultant ya nchini Bw. Robert (kulia) na
Mshauri wa Wanafunzi wa Education Placement Consultant Bi. Berinda.
Mwakilishi wa Taasisi ya Sta
Travel inayojihusisha na kusafirisha wanafunzi kwa punguzo ya gharama za
usafiri Bw. Abbas Karrim akisikiliza maoni kutoka kwa baadhi ya wadau
wa elimu waliotembelea meza yake katika maonyesho ya Tanzania
Internation Education Fair 2016 yanayoendelea katika Ukumbi wa British
Council jijini Dar es Salaam.
: Mwakilishi kutoka Chuo Kikuu
cha Eastern Medeterrenian cha nchini Uturuki akiwapa maelekezo wanafunzi
wakitanzania waliotembelea meza yake katika maonyesho ya Tanzania
Internation Education Fair 2016 yanayoendelea katika Ukumbi wa British
Council jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi kutoka Chuo Kikuu cha
Thompson cha nchini Canada Bi. Brenda Nicole akiwapa maelekezo wanafunzi
wakitanzania waliotembelea meza yake katika maonyesho ya Tanzania
Internation Education Fair 2016 yanayoendelea katika Ukumbi wa British
Council jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanafunzi wakipitia machapisho ya vyuo mbalimbali waliotembelea maonyesho ya Tanzania Internation Education Fair 2016 yanayoendelea katika Ukumbi wa British Council jijini Dar es Salaam.
Picha na Frank Shija
……………………………………………………………………………………………………………………
Na: Frank Shija, MAELEZO
Watanzania wanaosoma masomo ya
elimu ya juu nje ya nchi kunufaika na gharama ndogo zenye punguzo maalum
za kusafiri wakati wa kwenda na kurudi kutoka masomoni katika nchi
wanazo somea kupitia Taasisi ya Sta Travel ya jijini Dar es Salaam.
Hayo yamebainishwa na Mwakilishi
wa Taasisi ya Sta Travel Abbass Karim wakati wa monyesho ya Tanzania
International Education Fair 2016 yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Abbas amesema kuwa taasisi yao
imekuwa msaada mkubwa kwa Watanzania wanaopata fursa ya kusoma nje ya
nchi kwani wanatoa huduma ya usafiri ikiwa na punguzo maalum la gharama
za usafiri ili waweze kumudu gharama hizo.
Aliongeza kuwa mpaka sasa Taasisi
yake imetoa huduma ya hiyo kwa watanzania wengi nhasa wanafunzi
wanaoenda kusoma Kuala Lumpar Malyasia, London Uingereza, na Guangzhou
China.
Aidha Abbas alisema kuwa pamojja
na kutoa huduma hiyo kwa watanzania kumekuwa na changamoto katika
upatikanajji wa Viza kwa wateja wao na kupelekea kujitokeza kwa
usumbufu, hata hivyo Sta Travel imekuwa ikijitahidi kuwasaidia wateja
wake ili wakamilishe taratibu zao kwa wakati.
Kwa upande wake mtanzania
aliyenufaika na kupitia Taasisi hiyo Bw. Ally Abdallah amesema kuwa
binafsi anaipongeza taasisi hiyo kwa kuwa imemuwezesha kusafirikwa
gharama nafuu ambazo kwake zilikuwa rahisi kuzimudu tofauti na gharama
halisi ya usafiri kwa kawaida.
Sta Travel ni Taasisi
inayojihusisha na utoajji wa huduma ya kusafirisha wanafunzi kwa gharama
nafuu yenye punguzo maalum kwa leongo la kuwasaidia watanzania kufikia
ndoto zao bila kuwapo na kikwazo.


0 comments :
Post a Comment