Nkupamah Media
“Familia ya mpira wa miguu inajua umuhimu wa chanjo na hasa katika maendeleo ya vipaji na wanamichezo kwa
ujumla na jinisi chanjo inavyoweza kuwapa watoto siyo tu fursa ya maendeleo bali pia haki ya kuishi” ilisema sehemu ya barua hiyo iliyosainiwa na Rais wa TFF, Jamal Malinzi.
Katika barua hiyo, Malinzi ameelezea furaha ya TFF kuona kiongozi wa Tanzania akiongoza mapambano ya kuokoa afya na uhai wa kizazi cha sasa na kijacho katika Afrika na dunia kwa ujumla.
“TFF itaunga mkono juhudi zako ili kufanikisha malengo yaliyowekwa na ushirika wa chanjo” ilimalizia barua hiyo ambayo nakala yake imetumwa kwa Rais wa Caf, Issa Hayatou.


0 comments :
Post a Comment