Soma Habari Hii Uijue Imani Ya Afande Sele.Nikifa Nichomwe Moto Sihitaji Kuwa Binadamu Tena Nataka Kuwa Malaika -

Nkupamah Media:

Msanii Afande Sele ambaye anawakilisha mkoa wa Morogoro katika muziki amefunguka na kusema kuwa hataki kuja kuwa binadamu tena bali anahitaji kuwa Malaika.

Afande Selle alisema hayo kupitia kipindi cha Planet bongo cha East Africa Radio na kusisitiza kuwa siku atakayo kufa anaomba achomwe moto kwani yeye anaamini katika moto na si kuzikwa kawaida.
Afande Sele alidai kuwa amechoka kuwa binadamu bali anataka kuwa Malaika ndio maana anahitaji kuchomwa moto ili siku ya ufufuo arudi kama Malaika na si binadamu, imani yake inamtuma kuwa akizikwa kwenye udongo siku ya ufufuo atarudi kuwa binadamu tena jambo ambalo yeye hataki kusilisikia tena.

Kufuatia imani hiyo Afande Sele amesema mpaka sasa ameacha wosia kuwa siku atakayokufa achomwe moto na si kuzikwa.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment