WANANCHI WAMESHAURIWA KUACHA TABIA YA KULA KATIKA MAZINGIRA SI SALAMA

nKUPAMAH mEDIA:

imagesNa Magreth Kinabo –MAELEZO
……………………………………………
Wananchi wameshauriwa kuacha tabia ya kununua matunda yaliyomenywa barabarani au kula chakula kilichoandaliwa katika mazingira ambayo si safi na salama ili kuweza kuepuka ugonjwa kipindupindu na kulinda afya zao.
Kauli hiyo imetolewa leo na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto,Michael John wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dares Salaam kuhusu taarifa za ugonjwa huo kwa nchi nzima.
“Suala la kuepukana na ugonjwa wa kipindupindu linahitaji ushirikiano wa watu wote.Usiponunua matunda
yaliyomenywa na watu wanaouza barabarabani, hata wale wanaouza wataacha kuuza. Pia Serikali itatumia nguvu kidogo kwa ajili ya kuwadhibiti,” alisema John.
Akizungumzia kuhusu juhudi zinazofanyika za kukabialiana na ugonjwa huo, alisema hivi sasa kuna timu ya wataalamu ambayo imekwenda Morogoro ikiongozwa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dkt. Mpoki Ulisubisya na nyingine mkoani Dodoma ambayo itakuwa na Waziri wa wizara hiyo,Ummy Mwalimu ili kuweza kushirikiana na mamlaka, watendaji na baadhi ya wadau kuudhibiti ugonjwa huo.
Aliongeza kuwa ripoti ya ugonjwa huo kwa kipindi cha wiki jumla ya wagonjwa 459 wameripotiwa kuugua ugonjwa huo katika mikoa 15 na vifo vitano.
Alisema mkoa wa Simiyu ndio unaongoza kuwa na idadi ya wagonjwa wengi, ukifuatiwa na Mwanza, Mara na Morogoro. Pia mikoa ya Njombe , Ruvuma na Mtwara haijawahi kuripotiwa na ugonjwa huo.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment