Wamawake wakiwa wametandika
khanga kwenye wodi ya wazazi ya Hospitali ya Mkoa wa Mtwara, Februari
29, 2016.Waziri Mkuu, Kassim majaliwa alitembelea wodi hiyo na kukemea
mtindo huo akiwataka wauguzi na waganga kutandika mashuka yahospitali
ambayo alisema ana taarifa kuwa yapo ili kuepusha hatari ya wananwake
hao kubeba magonjwa kupitia kahanga hizo watokapo hospitalini
hapo.(Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
Wamawake wakiwa wametandika
khanga kwenye wodi ya wazazi ya Hospitali ya Mkoa wa Mtwara, Februari
29, 2016.Waziri Mkuu, Kassim majaliwa alitembelea wodi hiyo na kukemea
mtindo huo akiwataka wauguzi na waganga kutandika mashuka yahospitali
ambayo alisema ana taarifa kuwa yapo ili kuepusha hatari ya wananwake
hao kubeba magonjwa kupitia kahanga hizo watokapo hospitalini
hapo.(Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akitembelea hospitali ya Mkoa wa Mtwara Februari 29, 2016. Kushoto ni
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Halima Dendego na kulia Ni Mganga Mkuu wa
Hospitali hiyo, Dkt.Shaibu Maarifa.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akitembelea hospitali ya Mkoa wa Mtwara Februari 29, 2016. Kushoto ni
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Halima Dendego na kulia Ni Mganga Mkuu wa
Hospitali hiyo, Dkt.Shaibu Maarifa.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa
akizungumza na Waganga, Wauguzi na wafanyakazi wa Hospitali ya Mkoa wa
Mtwara wakati alipoitembelea Februari 29, 2016. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
Baadhi ya Wauguzi na Madaktari wa Hospitali ya Mkoa wa
Mtwara wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza
nao hospitalini hapo Februari 29, 2016. (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim majliwa
akitoa agizo la kusimamishwa kazi Daktari wa Hospitali ya Mkoa wa
Mtwara, Fortunatus Namahala (kulia) baada ya kutajwa kuwa alidai rushwa
ya sh.100, 000/= ili aweze kumtibu baba mzazi wa Tatu Abdallah (wapili
kulia) wakati alipoitembelea hospitali hiyo Februari 29, 2016. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa
akiagana na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Mtwara, Shaibu Maarifa
kwenye uwanja wa ndege wa Mtwara kabla ya kurejea Dar es slaam Februari
29, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim majaliwa akitazama ngoma kwenye uwanja
wa ndege wa Mtwara kabla ya kuondoka kurejea Dar es salaam Februari
29, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
………………………………………………………………………………………….
1.Ni baada ya kudai rushwa ya sh. 100,000/- kumfanyia upasuaji mgonjwa
2.Mama alilazimika kuuza shamba ili apate fedha za kumtibia baba yake
3.Aagiza maduka ya dawa nje ya hospitali hiyo yafungwe leo hii
4.Amwagiza RAS aitishe kikao cha watumishi wote leo saa 9 alasiri
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
ameagiza kusimamishwa kazi kwa Dk. Fortunatus Namahala wa kitengo cha
upasuaji katika hospitali ya Ligula ambayo ni hospitali mkoa wa Mtwara
kutokana na tuhuma za kumdai mgonjwa rushwa ya sh. 100,000/-.
Pia ametoa agizo la kufungwa kwa maduka yote ya dawa yaliyo nje
ya hospitali hiyo kuanzia leo na kumtaka Katibu Tawala wa Mkoa huo, Bw.
Alfred Luanda asimamie zoezi hilo mara moja.
Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo leo (Februari 29, 2016) kwenye
kikao cha watumishi wa hospitali hiyo alichokiitisha baada ya kutembelea
maeneo kadhaa ya hospitali hiyo na kupokea malalamiko kutoka kwa
wagonjwa na ndugu wenye wagonjwa waliolazwa.
Mara baada ya kuwasili, Waziri Mkuu aliamua kwenda mojamoja
mapokezi badala ya wodini kama alivyopangiwa na kuuliza maswali ni kwa
nini wana dirisha moja la kupokelea wagonjwa wote. “Dirisha la wazee
lipo?” akajibiwa hakuna. “Dirisha wa watu wa Bima ya Afya (NHIF) lipo”
nalo pia akajibiwa halipo. “Je wazee wana daktari wao”, hakupata jibu.
“Mganga Mkuu ni kwa nini
hujatenga dirisha la wazee wakati haya maelekezo yalishatolewa siku
nyingi? Tengeni dirisha la wazee na uhakikishe wana daktari wao. Siyo
kuwaleta huku ili waje kusukumana na wagonjwa vijana,” alisema wakati
akimwagiza Mgaga Mkuu wa Mkoa huo, Dk. Shaibu Maarifa.
Akiwa njiani kuelekea wodi
aliyopangiwa kuiona, Waziri Mkuu alikutana na kundi la wagonjwa
waliokuwa wakiimba “tuna jambo, tuna jambo” wakiashiria kutaka
kusikilizwa. Kati ya wauguzaji watatu aliowasikiliza, Waziri Mkuu
alipokea kero za kuuziwa dawa kwa bei za juu kwenye maduka ya dawa
binafsi, lugha mbaya za madaktari na wauguzi, uchafu wa vyoo na uhaba wa
maji.
Lakini kero ya Bi. Tatu Abdallah
aliyelazimika kuuza shamba la baba yake ekari 2.5 ili apate fedha za
kulipa gharama za kufanya upasuaji kwenye hospitali binafsi baada ya
baba huyo kutimuliwa kutoka hospitali ya Ligula ndiyo ilimgusa zaidi
Waziri Mkuu.
“Februari mosi nilimleta baba yangu hapa nikaambiwa anatakiwa
kufanyiwa upasuaji. Nikaandikiwa ninunuue dawa za sh. 85,000/- hapo nje
(pharmacy haikumbuki jina) pia uzi wa kushonea kwa sh. 25,000/-. Lakini
pia daktari akasema anataka sh. 100,000/- ya kwake. Lakini hadi Februari
7 hakufanyiwa huo upasuaji.”
“Tarehe 12 Februari baba alitolewa wodini na kuambiwa arudi
tarehe 16 Februari. Niliumia sababu kijiji tunachotoka ni mbali na hali
ya baba ilizidi kuzorota. Ndipo baba akaniambia nirudi kijijini kwetu
Kilomba nikauze ekari 2.5 za shamba lake ili tulipie matibabu. Niliuza
na kumpeleka baba katika zahanati ya Sajora. Huko nililipa sh. 560,000/-
na baba akafanyiwa upasuaji sasa hivi yuko nyumbani”.
“Leo nataka huyu daktari aje achukue boksi hili la dawa
alizoniandikia na pia anirudishie hela yangu iliyopotea bure. Mie
sijazitumia, ni kwa nini aliniandikia wakati baba hajampa huduma
yoyote?” Alipoulizwa kama anaweza kumtambua akimuona, mama huyo alikiri
kuwa anaweza.
Waziri Mkuu alitembelea pia wodi ya akinamama waliojifungua na
kukuta wakiwa wametandikiwa shuka moja na wagonjwa kulazimika kuweka
khanga juu ya mipira wanayolalia wodini ambayo pia wanaambiwa
wajinunulie kabla ya kwenda hospitali kujifungua.
Akiwa njiani kuelekea theatre, Waziri Mkuu alipata
kilio cha wagonjwa wengine ambao walisema hospitali hiyo haina maji,
choo kinachotumika ni kimoja na kwamba usafi umefanyika leo waliposikia
kuwa atatembelea hospitali hiyo.
Akiwa katika kikao na watumishi hao, Waziri Mkuu aliwainua
madaktari wote ili wajitambulishe ndipo akamuomba mama aliyedaiwa rushwa
aende kumshika mkono daktari mhusika.
“Gwaride la utambuzi ni jambo la kawaida. RPC hakikisha huyu
mama hasumbuliwi. Lakini leo nitaanza na huyu Daktari kwa sababu rushwa
haivumiliki. RAS simamia suala lake lakini pia shirikiana na TAKUKURU na
Polisi kufanya uchunguzi wa jambo hili hadi mwisho,” alisema.
Kuhusu madai na stahili za watumishi, Waziri Mkuu
amemwagiza RAS, RMO na Afisa Utumishi wa mkoa wafanye kikao na watumishi
wote wa hospitali hiyo leo saa 9 alasiri na kisha wamletee taarifa.
Kabla ya kufikia uamuzi wa
kumsimamisha Dk. Namahala, Waziri Mkuu alitumia muda mwingi kuwaelezea
watumishi hao jinsi walivyo na umuhimu katika huduma zao na kwamba
nafasi yao ni nyeti kwa maisha ya binadamu hivyo wanapaswa kuwa na
huruma na siyo kuwaumiza wananchi wa kipato cha chini ambao hawana uwezo
wa kumudu gharama za matibabu.
Aliwataka waache tabia ya
kuwatoza fedha watoto wanaolazwa hospitalini hapo na wanawake
wanaojifungua kwani wanapaswa kutibiwa bure kwa mujibu wa sera ya
Serikali.
Sakata la hospitali ya Ligula
lilianza juzi (Jumamosi, Februari 27, 2016) wakati Waziri Mkuu
akiwahutubia mamia ya wakazi wa Mtwara kwenye mkutano wa hadhara
uliofanyika katika uwanja wa mashujaa ambapo baadhi yao walikuwa
wakichomekea kuwa aende hospitalini hapo kwa kuwa kuna majipu ya
kutumbua.
Waziri Mkuu aliwajibu kuwa
amesikia ujumbe wao na ataenda huko lakini alishindwa kutokana na ratiba
za siku hiyo kumalizika jioni sana.
Waziri Mkuu amerejea Jijini Dar es Salaam mchana huu.
0 comments :
Post a Comment