Zoezi la kuhakiki watumishi hewa lililoamriwa na Rais John Magufuli limemkumba Askari Polisi aliyeajiriwa mwaka 2003 baada ya kubainika kuwa ametumia vyeti vya kugushi.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Zuberi Mwombeji amemtaja Askari huyo kuwa ni
Emanuel Nikolas Nyangoli mwenye namba F5425 Pc ambaye baada ya
kutuhumiwa kuwa na vyeti vya kughushi aliamua kutoroka na hajulikani
aliko.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Zuberi Mwombeji amesema Askari Emanuel Nyangol
amefanya kazi ndani ya jeshi la Polisi kwa muda wa miaka 13 bila
kujulikana kuwa ana vyeti vya kugushi,
Vielelezo
vya kuonyesha jeshi la polisi lina taarifa kuwa uajiriwa wa askari huyo
ni wakutatanisha ndio ulio mfanya atoroke baada ya kujua jeshi la
polisi lina taka kumfungulia mashitaka
Jeshi
la polisi mkoa wa Ruvuma linawaomba wanchi ambao watakuwa na tarifa za
Emanuel Nyangoli watoe tarifa kwa kituo chochote cha polisi au apige kwa
kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Nomber 0715 009 956.
0 comments :
Post a Comment