Kamati
ya Bunge ya Kudumu ya Maendeleo ya Jamii mapema Machi 29. 2016
imetembelea Makao makuu ya Bohari Kuu ya Dawa (MSD) kwa ajili ya
kujionea mambo mbalimbali ya kiutendaji na namna bohari hiyo inavyofanya
kazi katika kusambaza dawa zake hapa nchini.
Kamati
hiyo inaongozwa na Mh. Peter Serukamba (Mbunge) pamoja na wajumbe
mbalimbali wa kamati, wamepata kutembezwa katika maghala ya dawa yaliyo
kwenye bohari hiyo na kujionea hali halisi ikiwemo juhudi za Bohari hiyo
inavyopata dawa zake kutoka vyanzo tofauti tofauti pamoja na usambazaji
wake.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Maendeleo ya Jamii, Mh. Peter Serukamba
(wa kwanza kushoto) akifuatiwa na Mh. Suzan Lyimo (Mbunge wa Chadema).
Wengine ni Maofisa wa MSD, Kaimu Mkurugenzi wa Ugavi wa MSD, Bi. Mary
Ringo pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Manunuzi wa MSD, Bw. Fredrick
Nicolaus (kulia).
Kaimu
Mkurugenzi wa Ugavi wa MSD, Bi. Mary Ringo akitoa maelezo kwa Kamati ya
Bunge ya Maendeleo ya Jamii waliotembelea katika Bohari hiyo.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Maendeleo ya Jamii, Mh. Peter Serukamba
(wa kwanza kushoto) akifuatiwa na Mh. Suzan Lyimo (Mbunge wa Chadema).
Wengine ni Maofisa wa MSD, Kaimu Mkurugenzi wa Ugavi wa MSD, Bi. Mary
Ringo wakitembelea katika maghala hayo ya MSD.
Kamati hiyo ya kudumu ya Maendeleo ya Jamii ikitoka katika sehemu ya kuhifadhia dawa maalum ya hali ya ubaridi.
eneo la maghala ya MSD upande wa dawa maalum za miradi Msonge kama zinavyoonekana
Wabunge wakitoka katika ghala maalum la kuhifadhia dawa maalum za Msonge…
Mh.
Jacqueline Ngonyani (Mbunge) akitoka kuangalia moja ya mafriza
yanayohifadhia dawa maalum za matumizi ya kila siku wakati wa Wajumbe wa
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii.
Kaimu
Mkurugenzi wa Ugavi wa MSD, Bi. Mary Ringo akiwaonesha Waheshimiwa
Wabunge wa Kamati ya Maendeleo ya Jamii ya Bunge namna madawa
yaliyokwisha muda wake yanapohifadhiwa.
Baadhi ya madawa ambayo yamekwisha muda wake kama yanavyoonekana ndani ya maghala ya MSD
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla
akitoa ufafanui wa namna ya madawa hayo yanavyohifadhiwa katika maghala
hayo. kushoto ni Mbunge wa Viti Maalum, Mh. Jacqueline Ngonyani na
kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ha Maendeleo ya Jamii, Mh. Surukamba.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.
Hamisi Kigwangalla akiwaonyeshea wabunge namna dawa hizo
zinavyohifadhiwa katika mafriji maalum
Mbunge
wa Viti Maalum, Mh. Jacqueline Ngonyani akiuliza swali namna dawa
ambazo hazipewi kipaumbele kufikishwa katika vituo vya Afya.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Maendeleo ya Jamii, Mh. Peter Serukamba (kushoto)
akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mh. Hazzan Zungu.
Kamati hiyo ikielekea katika maghala ya kuhifadhia dawa ndani ya MSD.
Mkurugenzi
Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) Bwana Laurean Bwanakunu (katikati)
akijadiliana jambo na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla walipotembelea katika maghala
hayo.
Kaimu
Mkurugenzi wa Manunuzi wa MSD, Bw. Fredrick Nicolaus akiwaongoza Kamati
ya Maendeleo yaa Jamii kwenye maghala ya MSD wakati walipotembelea
bohari hiyo.
Baadhi
ya maafisa wa Wizara ya Afya na Bunge wakiwa kwenye msafara huo wa
Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii walipotembelea MSD.

Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.
Hamisi Kigwangalla akitoa maelezo namna ya maghala hayo yanavyohifadhi
dawa na namna ya kusambaza katika Hospitali za hapa nchini.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments :
Post a Comment