Kipindi cha redio cha Shuga charudi kwa kishindo

Mratibu wa Ukimwi kutoka Tume ya Kudhibiti ukimwi mkoa wa Njombe – TACAIDS   Abubakari Magege  akiongea na washiriki wa kipindi cha redio cha shuga katika uzinduzi rasmi wa msimu mpya wa kipindi hicho kitakachoanza kuruka tena katika redio mbalimbali nchini
Mwakilishi wa UNICEF   Alice Ijumba  akijibu maswali ya washiriki wa
wa kipindi cha redio cha shuga katika uzinduzi rasmi wa msimu wa pili wa kipindi hicho kitakachoanza kuruka tena katika redio mbalimbali nchini
 

 washiriki wa
wa kipindi cha redio cha shuga wakifuatilia mada kutoka kwa Mwakilishi wa UNICEF Alice Ijumba katika uzinduzi rasmi wa msimu mpya wa kipindi hicho kitakachoanza kuruka tena katika redio mbalimbali nchini
Alice Ijumba toka
UNICEF

Waratibu wa Shuga
Radio drama series msimu wa pili – Pendo Laizer na David
Sevuri wakichanganua ushiriki wa watangazaji na vikundi vya wasikilizaji

Mshiriki akichangia mada katika uzinduzi rasmi wa msimu mpya wa kipindi hicho kitakachoanza kuruka tena katika redio mbalimbali nchini;
Mratibu
wa Ukimwi kutoka Tume ya Kudhibiti ukimwi mkoa wa Iringa – TACAIDS,Fadhila
Mturi  akiongea na
waandishi wa habari mara baada ya ufunguzi wa semina elekezi
Vipindi vya redio vya
Shuga vitaanza kuunguruma tena kupitia redio mbalimbali nchini kuanzia wiki ya
pili ya mwezi wa nne mwaka huu. Vipindi hivyo vinalenga kuwaelimisha vijana
kuhusu maambukizi ya Virusi vya UKIMWI na UKIMWI, usawa wa jinsia, kufanya maamuzi
sahihi, matumizi sahihi ya kondomu na kuepukana na msongo rika.
Mfulilizo huu wa mchezo
wa redio wa Shuga unawalenga zaidi vijana hususan wasichana, kwa kuangalia
mtazamo wao, matarajio yao,  changamoto wanazopitia
ili kutimiza malengo yao na jinsi wanavyopambana na maisha yao ya kila siku.
Mchezo wa redio wa
Shuga ulianzishwa mnamo mwaka 2014 kwa ushirikiano kati ya MTV, HIV and AIDS
Free Generation, Shirika la TACAIDS pamoja na UNICEF. Baada ya mafanikio
makubwa msimu wa kwanza, TACAIDS na UNICEF pamoja na wadau wengine waliamua
kupanua wigo wa program hii kwa kuandaa vipindi zaidi ili kuimarisha tabia
chanya zilizojengwa katika msimu wa kwanza wa vipindi vya Shuga.
Katika kuboresha utoaji
elimu kuhusiana na mahudhui ya vipindi, mashirika ya UNICEF pamoja na TACAIDS
kwa kushirikiana na kampuni ya True Vision Production wanaendesha mafunzo elekezi
kwa vituo vya radio za jamii, mameneja wa radio shiriki, watangazaji na
waandishi wa habari pamoja na kwa waratibu wa UKIMWI ngazi za Halmashauri na
Mkoa, ambapo warsha hii inafanyika mkoani Iringa.
Radio zitakazoshiriki
katika urushaji wa vipindi vya Shuga msimu wa pili ni Clouds FM, Nuru FM –
Iringa, Kitulo FM – Makete, Kyela FM – Kyela pamoja na Furaha FM, Hope FM,
Qibla Ten FM za Iringa
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment