Mwakilishi
wa Shirika la UNFPA nchini Natalia Kanem (aliyesimama) akitoa hotuba ya
ufunguzi wa mafunzo ya kutumia simu kwa ajili ya kufundisha wakunga na
wauguzi njia ya uzazi salama, waliokaa kutoka kulia ni Mkurugenzi wa
Idara ya Mafunzo Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto (Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali) Dkt. Otilia Gowele, Msajili wa
Baraza la Uuguzi Lena Mfalila na Geeta Lal kutoka makao makuu ya UNFPA
Geeta
Lal kutoka Makao Makuu ya UNFPA akitoa maelekezo kwa washiriki (hawapo
pichani) kuhusu mafunzo ya uzazi salama ambayo yanapatikana ndani ya
simu hiyo.
Mkuu
wa Chuo cha Uuguzi Newala Tecla Ungele (wa kwanza kulia) akipokea seti
ya simu ya kufundishia uzazi salama kutoka kwa Mkurugenzi wa Idara ya
Mafunzo Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Otilia Gowelle , wa kwanza kushoto ni Mwakilishi wa Shirika la UNFPA
nchini Natalia Kanem
Mwalimu
wa Uuguzi Asha Ally Khamis (wa pili kulia) kutoka Chuo cha Afya Mbweni
Zanzibar akipokea simu ya kufundishia uzazi salama kutoka kwa Natalia
Kanem, wa kwanza kushoto ni Mwakilishi wa Shirika la UNFPA nchini na
Mkurugenzi wa Idara ya Mafunzo Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto. Dkt. Otilia Gowelle, kulia ni Nayanesh
Bhandutia kutoka makao makuu ya UNFPA.
Washiriki
wa mafunzo ya uzazi salama wakifuatilia kwa makini mafunzo kwa vitendo,
kutoka kushoto ni Mkufunzi Chuo Kikuu cha Muhimbili Dkt. Thecla Kohi,
Mratibu wa Mafunzo ya Wauguzi na Wakunga Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Vumilia Mmari na Annamagreth Mukwenda
kutoka taasisi ya MCSP (Maternal and Child Survival Program)
Washiriki
wa mafunzo ya uzazi salama kwa kutumia simu wakifuatilia jambo kwa
umakini kutoka kwa mwezeshaji (hayupo pichani) wa mafunzo hayo.
……………………………………………………………………………………..
Na Lilian Lundo-MAELEZO
Shirika la Maendeleo la Umoja wa
Mataifa (UNFPA) limekabidhi simu za kufundishia huduma ya uzazi salama
kwa vyuo vya Afya pamoja na taasisi zinajihusisha na masuala ya afya ya
mama na mtoto ili kuboresha huduma kwa akina mama wajawazito na watoto
wanaozaliwa.
Makabidhiano hayo yamefanyika
jijini Dar es Salaam Machi 21, 2016 baina ya shirika la UNFPA na Wizara
ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
Akikabidhi vifaa hivyo Mwakilishi
wa Shirika la UNFPA nchini Natalia Kanem alisema wanashirikiana na
Serikali ya Tanzania katika kukuza na kuboresha elimu juu ya uzazi
salama na kupunguza vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua.
“Dhumuni la matumizi ya simu za
kufundishia uzazi salama ni kutoa elimu kwa wauguzi na wakunga walioko
vijijini na maeneo ambayo hayafikiki kwa urahisi ili kuwasaidia kupata
elimu ya uzazi salama na kupunguza vifo vya mama na mtoto,” alisema
Natalia.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa
Idara ya Mafunzo Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Dkt. Otilia Gowele ambaye alimwakilisha Mganga Mkuu wa Serikali
alisema kuwa simu hizo zitarahisisha ufundishaji kwa wauguzi na wakunga
kwani zitawawezesha kujifunza masuala yote yanayohusu uzazi salama bila
kuondoka kwenye vituo vyao vya kazi.
Dkt. Gowele aliongeza kwa kusema
kuwa, simu hizo zitakuwa na mafunzo ya uuguzi ambayo yako katika mitaala
ya vyuo vya uuguzi na mtumiaji wa simu hiyo anaweza kuuliza swali
lolote linalohusu uzazi salama akapata majibu kwa njia ya sauti, picha
na maandishi.
Aidha, simu hizo zinachajiwa kwa
kutumia umeme wa mwanga jua, umeme wa wakawaida na inatumia betri pia,
hivyo inaweza kutumika hata maeneo ambayo bado hayajafikiwa na umeme.
Kwa upande wake Mtaalamu wa Afya
ya Mama na Mtoto wa UNFPA Felister Bwana alisema kuwa, simu hizo
zimegawiwa kama majaribio kwa baadhi ya vyuo vya Afya na na taasisi
zinazojihusisha na uzazi salama, endapo teknolojia hiyo italeta
mafanikio yanayotarajiwa simu hizo zitagawanywa kwa vyuo vyote vya
uuguzi na hospitali nchini.
Vyuo na taasisi ambavyo vimepokea
vifaa hivyo ni pamoja na Chuo cha Afya Kilosa, Bugando, Newala,
Nachingwea, Bagamoyo, Geita, Kahama, Maswa, Sengerema, KCMC, Zanzibar,
Ifakara pamoja na taasisi ya TAMA na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto.
Kwa mujibu ya sensa ya mwaka 2010,
jumla ya vifo 454 vimekuwa vikitokea katika kila vizazi hai 100,000
kwa mwaka, idadi hiyo imepungua na kufikia vifo 432 kwa kila vizazi hai
100,000 kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012.


0 comments :
Post a Comment