Mshambuaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo usiku wa jana, amefikisha idadi ya magoli 90 ambayo ameshafunga katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA) katika historia yake ya maisha ya soka.
Ronaldo alifunga goli la 90 katika mchezo wa pili wa hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Roma katika dakika ya 64 na baadae kutengeneza goli la pili kwa Real Madrid kwa kutoa pasi ya mwisho kwa James Rodriguez dakika ya 68.
Aidha goli alilofunga Ronaldo limekuwa goli lake la 13 katika Ligi ya Mabingwa kwa msimu huu na goli la 40 katika mashindano yote ameyocheza kwa msimu huu.



0 comments :
Post a Comment