Akihutubia katika uzinduzi wa
Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Rais wa Zanzibar Dr Ali Mohamed Shein
amesema kuwa kwenye uchaguzi wa Marudio uliofanyika Machi 20, hakuna
chama kilichopata kura za rais kwa zaidi ya asilimia 10 isipokuwa CCM.
Pia amesema kuwa hakuna chama kilichopata wabunge wengi isipokuwa CCM.
Kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar,
hakuna chama kilichopewaa ridhaa ya kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa
isipokuwa CCM. Kwamba, Makamu wa Pili amechaguliwa kwa mujibu wa sheria
na hakuna nafasi Kikatiba ya kuteua Makamu wa Kwanza wa Rais ama
Mawaziri kutoka Upinzani. Amesema hayo ni maamuzi ya wananchi na ni
lazima yaheshimiwe. Wananchi Wamewakataa wapinzani na kuiamini CCM. Kwa
hali hiyo ni kwamba Serikali ya Umoja wa Kitaifa imekufa rasmi
0 comments :
Post a Comment