
Mkurugenzi
 Mkuu wa Maxmalipo  Juma Rajabu akifafanua jambo kwa wakurungezi wa 
serikali za mitaa kutoka Uganda , Kulia ni Mkuu wa Uendeshaji Kanda 
Group COO – Maxcom Africa Jamson Kassati , Kushoto Mwanzo Mr. Moses 
Kimaro Kutoka ALAT (jumuiya ya serikali za MItaa Tanzania)  na pembeni 
yake katikati ni Mwenyekiti wa wakurugenzi wa Serikali za Mitaa Kutoka 
Uganda Dunstan Balaba ambapo Jumuiya hiyo ya wakurugenzi wa serikali za 
Mitaa wapatao 60 Kutoka Uganda leo wametembelea Ofisi za Maxmalipo 
Kujifunza ni jinsi Gani kampuni hii imeweza kugundua teknolojia 
inayosaidia kudhibiti makusanyo kwenye vyanzo mbalimbali vya mapato 
katika Halmashauri za miji na majiji Nchini Tanzania.

Mkuu wa 
Kitengo cha Biashara Kutoka Maxmalipo Bw. Deogratius Lazari Akifafanua 
Jambo kwa Wakurugenzi hawa kutoka Uganda, Akielezea Jinsi mfumo wa 
Ukusanyaji Kodi na tozo mbalimbali ulivyorahisisha upatikanaji wa mapato
 katika halmashauri mbalimbali na Taasisi za Serikali kwa Ujumla na 
kuzuia mianya ya upoteaji wa mapato katika vyanzo mbalimbali vya 
halmashauri.

Mwenyekiti na Msemaji wa Umoja wa wakurugenzi kutoka Uganda Bwana Dunstan Balaba Akieleza Jambo kwa Hadhara na Kukiri kushangazwa na watanzania Kuweza Kugundua Teknolojia kama hii. Pia Kumwomba Mkurugenzi wa Maxmalipo Afungue Ofisi Uganda Mapema iwezekanavyo.

Wakurugenzi
 wa Serikali za Mitaa Kutoka UGANDA wakifuatilia Mada Kutoka kwa Mkuu wa
 Kitengo cha Biashara wa Kampuni ya Maxmalipo  Bw. Deogratius Lazari 
ambapo Mkurugenzi Mkuu wa Maxmalipo  Juma Rajabu anasema; Safari ya 
kuuaminisha Umma na Serikali kwamba wazawa wanaweza kubuni mbinu 
mbalimbali za kusaidia kuboresha makusanyo, inaenda sambamba na ufanisi 
mzuri uliothibitika katika  kazi mbalimbali ambazo kampuni Imekua 
ikizifanya, Juma Rajabu ameongeza kwa kuelezea jinsi ambavyo teknolojia 
imerahisisha ulipajji wa bili mbalimbali Ikiwamo Luku, Kodi za TRA, 
Ving’amuzi na hata ukusanyaji wa mapato kwenye vivuko.

Mmoja Wa 
wakurugenzi kutoka Uganda Bibi Lilian Akiuliza Swali kwa Maxmalipo 
wakati Jumuiya hiyo ya wakurugenzi wa serikali za Mitaa wapatao 60 
Kutoka Uganda leo wametembelea Ofisi za Maxmalipo Kujifunza ni jinsi 
Gani kampuni hii Imeweza kuugundua teknolojia inayosaidia kudhibiti 
makusanyo kwenye vyanzo mbalimbali vya mapato katika Halmashauri za miji
 na majiji Nchini Tanzania. 
Jumuiya 
 ya wakurugenzi wa serikali za Mitaa wapatao 60 Kutoka Uganda wakiwa 
katika picha ya pamoja na viongozi wa kampuni ya MAXCOM Africa  mapema 
 leo walipokuwa wametembelea Ofisi za Maxmalipo Kujifunza ni jinsi Gani 
kampuni hii Imeweza kugundua teknolojia inayosaidia kudhibiti makusanyo 
kwenye vyanzo mbalimbali vya mapato katika Halmashauri za miji na majiji
 Nchini Tanzania


0 comments :
Post a Comment