Donald Trump
Mgombea
wa urais nchini Marekani kwa tiketi ya chama cha Republican Donald Trump
ameahidi kubadilisha sifa zake katika mkutano wa faragha na viongozi wa
Republican.
Mfanyibishara
huyo ambaye yuko kifua mbele katika kuwania urais kupitia chama hicho
alitoa ujumbe wake kupitia wasaidizi wake ,kulingana na chombo cha
habari cha AP.
Kuimarika
kwake katika mchujo huo kufikia sasa kumetuma ishara miongoni mwa
viongozi wa chama hicho kwamba matamshi pamoja na sera zake huenda
zisiwavutie wapiga kura.
Majimbo matano yanapiga kura siku ya Jumanne kumchagua mgombea wao wa urais.
Bwana
Trump ana uongozi mkubwa wa idadi ya wajumbe lakini huenda asipate
wajumbe 1,237 anaohitaji kushinda mchujo huo bila ya mkutano wa
wanachama.
Wasaidizi wamewaambia viongozi wa chama kwamba amekuwa akibadilisha sifa zake na kwamba hatua hiyo imeanza kufua dafu.

0 comments :
Post a Comment