Mchezaji nyota wa zamani wa timu
ya taifa ya Naijeria, Nwanko Kanu ambaye kwa sasa ni balozi wa makampuni
ya StarTimes barani Afrika akiwaelekeza watoto katika mafunzo ya mpira
wa miguu wakati alipotembelea katika kituo cha michezo ya Jakaya Kikwete
kilichopo Kidongo Chekundu jijini Dar es salaam.
Mchezaji nyota wa zamani wa timu
ya taifa ya Naijeria, Nwanko Kanu ambaye kwa sasa ni balozi wa makampuni
ya StarTimes barani Afrika akiwaelekeza watoto katika mafunzo ya mpira
wa miguu wakati alipotembelea katika kituo cha michezo ya Jakaya Kikwete
kilichopo Kidongo Chekundu jijini Dar es salaam.
Mchezaji nyota wa zamani wa timu
ya taifa ya Naijeria, Nwanko Kanu ambaye kwa sasa ni balozi wa makampuni
ya StarTimes barani Afrika akizungumza na watoto mara baada ya mafunzo
ya mpira wa miguu wakati alipotembelea katika kituo cha michezo ya
Jakaya Kikwete kilichopo Kidongo Chekundu jijini Dar es salaam.
Mchezaji nyota wa zamani wa timu
ya taifa ya Naijeria, Nwanko Kanu ambaye kwa sasa ni balozi wa makampuni
ya StarTimes barani Afrika akizungumza na watoto mara baada ya mafunzo
ya mpira wa miguu wakati alipotembelea katika kituo cha michezo ya
Jakaya Kikwete kilichopo Kidongo Chekundu jijini Dar es salaam.
………………………………………………………………………………………
Mchezaji nyota wa zamani wa timu
ya taifa ya Nigeria, Nwanko Kanu ambaye kwa sasa ni balozi wa makampuni
ya StarTimes barani Afrika ametembelea na kushiriki kwenye mafunzo na
watoto kwenye kituo cha Jakaya Mrisho Kikwete cha jijini Dar es Salaam
mwishoni mwa wiki.
Kanu ambaye amekuja kwa shughuli
za kampuni hiyo atakuwepo nchini Tanzania kwa muda wa siku tano
alifurahi sana kuona watoto wameandaliwa mazingira mazuri kwa ajili ya
michezo mbalimbali kwani sio wote waliopata fursa hiyo.
“Wakati mimi ninaanza kucheza
mpira hakukuwa na kituo kizuri kama hiki wala jezi, viatu na walimu
wazuri mlio nao sasa. Hii ni fursa ya kipekee kwenu nyinyi kuweza
kuonyesha juhudi za kujifunza ili mje kuwa kama mimi siku za mbeleni.
Leo mimi nimekuwa maarufu ni kwa sababu nilikuwa na nidhamu, bidii,
dhamira na kuwasikiliza walimu wangu walipokuwa wananifundisha. Hatimaye
leo hii nina mafanikio makubwa, ninaishi maisha mazuri, wazazi wangu
pia wanaishi mahali pazuri, wanasafiri na kupata wanachokitaka kwa
sababu tu ya mimi kufanikiwa.” Kanu aliwaambia watoto wa kituo cha
Jakaya Kikwete
Kampuni ya StarTimes ambayo imo
zaidi ya nchi kumi barani Afrika imemtua mchezaji huyo kama balozi
katika kuwawakilisha katika shughuli mbalimbali. Kanu anatarajia kuwa
chachu kwa katika kampuni hiyo hususani katika kuboresha na kuongeza
vipindi na chaneli za michezo kwani waafrika wengi wanapenda soka.
“Ninaamini mchezo wa soka ndio
unaopendwa na watu wengi zaidi duniani na waafrika ni miongoni mwao.
StarTimes mpaka sasa wamepiga hatua kubwa katika kulisimamia hili, mpaka
sasa tayari wana haki miliki za kuonyesha ligi za Budensiliga na Serie A
za Ujerumani na Italia. Hiyo ni hatua kubwa kwani wateja wanafurahia
michezo hiyo inyoonekana moja kwa moja kwa vifurusushi vya bei nafuu.
Kama balozi ninaahidi kushirikiana na kampuni katika kuboresha zaidi
vipindi vyake na pia kuishauri kujikita zaidi na michezo ya nyumbani.
Kama mnavyoona kwa mara ya kwanza tumedhamini ligi daraja la kwanza.”
Aliongezea mchezaji Kanu
Kanu alihitimisha kwa kuwataka
watoto wa kituoni hapo kuonyesha bidii, utii na dhamira ya dhati kwa
kila wanachokifanya, “Ningependa kuwashauri wadogo zangu kuwa popote
utakapokwenda duniani kwenye mchezo wa soka, viwanja na mipira
inayotumika ni hii hii wala hakuna tofauti yoyote. Hivyo basi sioni kama
kuna kitu cha kuwazuia na nyinyi msifanikiwe. Kama nilivyowaambia
awali, bidii, nidhamu, dhamira na utii kwa walimu wenu ndio msingi wa
mafanikio ya mwanasoka yeyote Yule duniani. Nawatakia kila la kheri na
siku nyingine nikija Tanzania naahidi kuwatembelea tena.”
Naye kwa upande wake Kocha Mkuu
wa Kituo cha Vijana cha Jakaya Mrisho Kikwete, Bw. Eduard Tamayo
alielezea furaha yake kwa kampuni ya StarTimes kuandaa kitu kama hiko na
kukiteua kituo hiko kuwa mwenyeji wa ugeni wa Kanu nchini Tanzania.
“Nimefurahi sana kwa ujio
aliyekuwa mchezaji wa timu ya taifa ya Naijeria na vilabu vikubwa barani
Ulaya kama vile Ajax, Inter Milan na Arsena, Nwanko Kanu kutembelea
hapa na kushiriki mafunzo na watoto. Hii ni bahati kubwa sana kwa watoto
hawa kwani ni nadra sana kutokea, kupata mafunzo, kuzungumza, kupata
ushauri na kuuliza maswali moja kwa moja kwa Kanu. Ninatumaini itakuwa
imewapa motisha kubwa sana.” Alisema Bw. Tamayo
Kocha Mkuu huyo kituoni hapo
alihitimisha kwa kuwataka wazazi kuwapeleka na kuwasajili watoto kituoni
hapo kwa mafunzo kwani wanapokelewa na kuwapatia mafunzo mazuri kwa
kuviendeleza vipaji vyao. Na kwamba kituo hiko ni fursa kwa watanzania
hivyo ni vema kukitumia vizuri.


0 comments :
Post a Comment