Tanzania
na Burundi zimeombwa kulegeza misimamo yao kwa kuondoa gharama za
vibali vya kufanya kazi kwa raia wa nchi zinazounda jumuia ya Afrika
Mashariki (EAC) kama zilivyofanya nchi za Rwanda, Uganda na Kenya ambazo
nazo ni wanachama wa jumuiya hiyo.
Akizungumza
jijini Arusha hivikaribuni Katibu wa Chama cha Waajiri Afrika Mashariki
(EAEO), Aggrey Mlinuka alisema kuwa hadi sasa nchi za Tanzania na
Burundi ndizo nchi pekee zilizobakia katika kutoza gharama za vibali vya
wageni hasa raia wa Jumuia ya Afrika Mashariki.
Mlimuka
alisema kuwa mbali na nchi hizo kuondoa utaratibu huo pia amependekeza
kwamba utaratibu wa utoaji vibali hivyo usichukua muda mrefu kama ilivyo
sasa kwa nchi za Tanzania na Burundi na kushauri muda wa kuchukua
vibali hivyo haustahili kuzidi siku 30.
Katibu
huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha waajiri Tanzania (ATE)
alisema kuwa chama chao kiliwasilisha mapendekezo hayo mbele ya Katibu
Mkuu wa Jumuia ya Afrika Mashariki, Dk. Richard Sezibera ambaye
anamaliza muda wake April 20 mwaka huu.
“EAEO
na Sezzibera tumefanya kazi kubwa kuhakikisha jumuiya inasonga mbele
kwa kasi kubwa mbali na changamoto zilizopo katika nchi moja moja,
lakini tuna uhakika tutazitatua kwa manufaa na maslahi ya wana jumuiya
wote,” alisema Mlinuka.
Alisema
kuwa Katibu Mkuu mpya Liberata Mfumukeko kutoka kutoka Burundi
anatakiwa kuendeleza pale ambapo Dk Sezzibera anapoishia ambapo ni
kuhakikisha kwamba unakuwepo utatu wa ajira katika jumuiya ya Afrika
Mashariki.
Mbali
na hilo pia amemtaka katibu mkuu huyo mpya kuhakikisha protokali ya
soko la pamoja kipengele cha pili cha jumuia ya Afrika Mashariki
kinatekelezeka ikiwa ni pamoja na kuondoa vikwazo vya wananchi
kuingiliana kutoka sehemu moja kwenda nyingine kibiashara pamoja na
kutafuta ajira ndani ya nchi wanachama.
Awali
Mwenyekiti wa chama cha waajiri Kenya(FKE) Jacqueline Mugo alisema kuwa
nchi wanachama hazipaswi kuwa na uoga katika yale ambayo yanaonekana
kuwa na manufaa na uhai wa Jumuia ya Afrika Mashariki yakiwemo masuala
ya ajira na mengineyo.
Mkutano
wa siku moja ulikutanisha vyama vyote vya waajiri wa nchi zinazounda
jumuia ya Afrika Mashariki vikiwa na malengo ya kuhakikisha wananchi wa
jumuiya hiyo wanapata ajira popote pale wanapokwenda ndani ya jumuiya ya
Afrika Mashariki.
0 comments :
Post a Comment