Beki
wa kulia wa timu ya soka ya Young African ya Dar es Salaam, Juma Abdul
(kulia pichani juu) )ameteuliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Aprili, 2016
baada ya kura zake kuwashinda Donald Ngoma ambaye pia anakipiga Young
Africans na Hassan Dilunga wa JKT Ruvu ya Pwani.
Katika
rekodi za Bodi ya Ligi Tanzania Bara (TPLB) iliyoketi Jumamosi
Iliyopita, imeonesha kwamba Abdul alicheza mechi zote tano za Ligi Kuu
kwa mwezi Aprili ambapo pia aliifungia timu yake bao katika harakati za
kuwania ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2015/16.
Rekodi
hizo pia zinaonyesha kwamba beki huyo hakuonyeshwa kadi hata moja
katika michezo hiyo mitano sambamba na kutoa mchango mkubwa katika
michezo aliyoshiriki kwa mwezi Aprili, 2016. Abdul atazawadiwa fedha Sh.
1,000,000 (milioni moja) na wadhamini wa Ligi hiyo, Kampuni ya mahiri
ya simu za mkononi ya Vodacom.
Uwezo
aliouonyesha Abdul ulisababisha Kocha wa Taifa Stars, Charles Boniface
Mkwasa ‘Master’ kumjumuisha katika kikosi chake kwa ajili ya mechi ya
kirafiki ya kimataifa dhidi ya Harambee Stars ya Kenya kadhalika
Mapharao wa Misri katika mechi ya kuwania kufuzu fainali za Kombe la
Mataifa ya Afrika utakaofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Juni 4,
mwaka huu.
Wachezaji
bora wa miezi minne iliyopita ni kiungo Thaban Kamusoko wa Young
Africans (Desemba 2015), beki Shomari Kapombe wa Azam (Januari 2016),
Mshambuliaji Mohamed Mkopi wa Tanzania Prisons (Februari 2016) na Shiza
Ramadhani Kichuya wa Mtibwa Sugar (Machi 2016).
Blogger Comment
Facebook Comment