Rais
wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Gianni Infantino (Pichani
juu) ameipongeza timu ya soka Young Africans ya Dar es Salaam (Pichani
chini) kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara 2015/16.
Young
Africans imetwaa ubingwa huo kwa msimu wa pili mfululizo, lakini ikiwa
ni mara ya 26 tangu kuanza kwa Ligi Kuu Bara mwaka 1965.
Katika
salamu zake, kupitia barua yake ya Mei 18, 2016 kwa Rais wa Shirikisho
la Soka Tanzania (TFF), Jamal Emil Malinzi, Infantino ameelezea ubingwa
wa Young Africans kwamba umetokana na kazi kubwa inayofanywa na uongozi
wa timu hiyo, makocha, wachezaji pamoja na mashabiki.
“Yanga
ndiyo mabingwa wa Tanzania. Napenda kuchukua nafasi hii kuipongeza
Young Africans na timu nzima isiyoshindika kwa mafanikio haya makubwa.
Taji la Young Africans ni matokeo ya mshikamano ulioko ndani ya Young
Africans,” amesema Infantino katika barua hiyo yenye kichwa cha habari
kinachosema: Salamu za Pongezi kwa Young Africans.
Amesema
pongezi zake ziende kwa uongozi wa klabu, makocha na benchi nzima la
ufundi, wachezaji, madaktari pamoja na mashabiki wote wa Young Africans.
“Kwa
niaba ya familia ya soka, napenda kuchukua nafasi hii kuishukuru Young
Africans na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa jinsi mnavyopeleka
ujumbe chanya wa soka kwa jamii ya michezo,” alisema Infantino katika
barua hiyo iliyotua TFF Mei 21, mwaka huu.
Tayari
Rais wa TFF, Jamal Malinzi alikwisha kuipongeza Yanga ambayo imepewa
Kombe na medali kwa wachezaji 24, viongozi saba wa benchi la ufundi na
viongozi wanne wa Kamati ya Utendaji na kwa sasa wanasubiri zawadi ya
fedha Sh 81,345,723.
Blogger Comment
Facebook Comment