Teddy Cruz wa chama cha Republican
Seneta wa
jimbo la Texas Ted Cruz amejiondoa katika kinyanganyiro cha uteuzi
kugombea nafasi ya urais wa Marekani kupitia chama cha Republican.
Alitoa
tangazo lake punde tu baada ya kupoteza kura katika kampeni za mwisho
Indiana.Cruz amewaambia wafuasi wake kuwa alifanya kila analoweza katika
kampeni zake,lakini hakukuwa na njia ya yeye kuweza kusonga mbele
zaidi.
Mwandishi
wa BBC aliyepo katika vituo vya kupigia kura Indiana amesema wafuasi wa
Cruz wamestushwa na kukatishwa tamaa.Tangazo hilo linatoa mwanya kwa
Donald Trump kupata uteuzi wa chama chake cha Republican.
Chanzo:BBC
0 comments :
Post a Comment