Rais wa Ufilipino, Benigno Aquino katika kambi ya jeshi la anga, Angeles city, Pampanga DIsemba 21,2015.
Na RFI
Kundi la
wanamgambo wa Kiislamu la Abu Sayyaf limerusha hewani Jumanne hii video
inayowaonyesha mateka watatu, kutoka Canada, Norway na Ufilipino, na
kutishia kuwaua, wiki mmoja baada ya kumua raia moja wa Canada
aliyetekwa nyara pamoja nao.
Katika
video hiyo, iliyorushwa Jumanne hii kwenye YouTube,mateka hao watatu
tatu, kutoka Canada Robert Hall, Norway Kjartan Sekkingstad, na
Ufilipino Marites Flor, rafiki wa Bw Hall, wametoa wito kwa serikali za
Canada na Ufilipino, wakiomba "kutekeleza madai ya kundi hilo", shirika
maalum katika ufuatiliaji wa vyombo vya habari vya jihadi SITE,
limearifu.
Mateka
hao wameonekana wakikaa chini, nyuma ya shamba la linaloonekana kuwa la
nazi, chini ya ulinzi wa watu sita wenye silaha wakisimama nyuma yao.
Mateka
kutoka Canada, Robert Hall, anasema watekaji nyara wamemuamuru kuomba
serikali ya Canada na "kutekeleza" mahitaji yao, bila kuyabainisha.
Mateka
kutoka Norway, Kjartan Sekkingstad, amesisitiza kwamba kama "madai hayo
hayatotekelezwa, tutauawa siku chache kama rafiki yetu John."
Mmoja wa
watekaji nyara ameonya serikali ya Ufilipino naupata "somo" katika
mauaji ya John Ridsdel na kuepukakuchelewa katika mazungumzo hayo.
Kundi
hili wanamgambo wa Kiislamu la Abu Sayyaf lilitangaza wiki iliyopita
kuwa lilimuua mateka kutoka Canada John Ridsdel, baada ya kumalizika kwa
muda uliyotolewa Aprili 25, kwa kutoa fidia ili aweze kuachiliwa huru.
Mateka
hawa watatu walitekwa nyara mwishoni mwa mwezi Septemba pamoja na John
Ridsdel, walipokuwa katika mgahawa kusini mwa Ufilipino.
Rais
Ufilipino Benigno Aquino aliahidi mwishoni mwa mwezi Aprili kuanzisha
mashambulizi ya kijeshi kwa lengo la "kutokomeza shughuli za kihalifu"
za kundi la Abu Sayyaf na kuonya kuwa serikali haitojadiliana na shirika
inalolichukulia kama la kigaidi.
Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau pia ametupilia mbali mazungumzo yoyote na watekaji nyara.
Bw Aquino
alisema kuwa mateka wanashikiliwa katika kisiwa cha Jolo, ngome kuu ya
jadiya kundi la Abu Sayyaf, zaidi ya kilomita elfu kusini mwa Manila.
0 comments :
Post a Comment