Spika wa
Bunge Mhe. Job Ndugai akilihutubia Bunge la Afrika (Pan African
Parliament) kuwasilisha Ujumbe wa Mshikamano kwa wabunge wa Bunge hilo
wakati wa Ufunguzi wa rasmi wa Mkutano wa Pili wa Bunge hilo uliofanyika
Mjini Midrand Afrika Kusini. Mhe. Ndugai alikuwa miongoni mwa viongozi
mashuhuri 12 kutoka Barani Afrika walioalikwa kutoa ujumbe huo kwa
wabunge wa Afrika.
Spika wa
Bunge Mhe. Job Ndugai akilihutubia Bunge la Afrika (Pan African
Parliament) kuwasilisha Ujumbe wa Mshikamano kwa wabunge wa Bunge hilo
wakati wa Ufunguzi wa rasmi wa Mkutano wa Pili wa Bunge hilo uliofanyika
Mjini Midrand Afrika Kusini. Mhe. Ndugai alikuwa miongoni mwa viongozi
mashuhuri 12 kutoka Barani Afrika walioalikwa kutoa ujumbe huo kwa
wabunge wa Afrika.
Spika wa
Mhe. Job Ndugai akiwa na baadhi ya Maspika wenzie kutoka mabunge ya Nchi
za Bara la Afrika kwenye Mkutano wa Bunge la Afrika (Pan African
Parliament) alikoalikwa kuwasilisha Ujumbe wa Mshikamano kwa wabunge wa
Bunge hilo wakati wa Ufunguzi wa rasmi wa Mkutano wa Pili wa Bunge hilo
uliofanyika Mjini Midrand Afrika Kusini. Mhe. Ndugai alikuwa miongoni
mwa viongozi mashuhuri 12 kutoka Barani Afrika walioalikwa kutoa ujumbe
huo kwa wabunge wa Afrika. Kulia kwake ni Spika wa Bunge la Seneta la
Lesotho Mhe Seeiso Berenge Seeiso na kushoto ni senate kutoka Bunge la
Afrika Mhe. Bennette hayatoe (P.T)
Wabunge
wa Bunge la Afrika wanaowakilisha Tanzania wakila kiapa cha uaminifu.
Kutoka kushoto ni Mhe. Asha Abdalah Juma, Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile,
Mhe. David Silinde na Mhe. Mboni Mhita.
Na Owen Mwandumbya, Midrand Afrika Kusini.
Spika wa
Bunge la Tanzania Mhe. Job Ndugai amesema ili Bara la afrika liweze kuwa
Bara lenye nguvu kiuchumi na sauti ya maamuzi duniani halina budi
kujikita katika umoja na mshikamono.
Mhe.
Ndugai aliyasema hayo alipokuwa akilihutubia Bunge la Afrika (Pan
African Parliament) leo kuwasilisha Ujumbe wa Mshikamano kwa wabunge wa
Bunge hilo wakati wa Ufunguzi wa rasmi wa Mkutano wa Pili wa Bunge hilo
uliofanyika Mjini Midrand Afrika Kusini.
Akizungumzia
changamoto zinazolikabli bara la Afrika Mhe. Nduagi alisema nchi nyingi
barani Afrika zinakabiliwa na matatizo yanayolingana ambayo ni Vita vya
wenyewe kwa wenyewe, ugaidi, umasikini na mengineyo ambayo yanahitaji
suluhisho la Pamoja kuyakabili..
“ katika
duniani ya sasa ni vyema tukakabiliana na changamoto zinazotukabili kwa
pamoja. Matajiri hawawezi kuepuka athari za umasikini na ukosefu wa
amani. Kinachotokea eneo moja kinaathiri maeneno mengi mathalani vita
vya wenyewe kwa wenyewe Somalia imesababisha wakimbizi katika maeneo
mengi duniani” alisema Ndugai
Akizungumzia
nafasi ya wabunge katika kupiga vita changamoto zinazolikabili bara la
Afrika, Mhe. Ndugai amesema wabunge wa Bunge la Afrika kama wawakilishi
wa Manbunge ya Nchi wanachama wa Umoja wa Afrika wanawajibu wa kutetea
maslahi ya Bara la Afrika bila kujali itikadi za kisiasa, maeneo
wanayotoka na mambo mengine yanayoweza kuligawa bara la Afrika.
“ Mkiwa
Wabunge mnaowakilisha nchi zenu katika Bunge hili, nilazima mhakikishe
Umoja wa Afrika unasimamia ipasavyo masalahi ya bara la Afrika ili
kutimiza ndoto waliokuwa nayo waasisi wa umoja huu wa Afrika. Kwa mfano
baba wa Taifa la Tanzania Mwalimu Julius kambarage Nyerere alisema
lazima tukimbie wakati wengine wakitembea” aliongeza Ndugai
Mapema
akitoa salamu za Bunge la Lesotho, Spika wa Bunge la Nchi hiyo Mhe.
Nthloi Motsamai alisifu juhudi za Mwalimu Julius Nyerere pamoja na
waasisi wengine wa bara hili katika kuimarisha umoja wa Afrika na
kuwataka wabunge wa Bunge la afrika kuhakikisha mawazo ya viongozi hawa
ya kulifanya bara la afrika kuwa moja yanatimia.
Katika
hatua nyingine, wabunge wa Tanzania wanaowakilisha Tanzania katika Bunge
la Afrika walikula kiapo cha uaminifu kuwa wabunge wa Bunge hilo baada
ya Bunge la Tanzania kuwachagua mapema mwezi Januari.
Wabunge
hao ni pamoja na Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile, Mhe. Mboni Mhita, Mhe.
David Silinde na Mhe. Asha Abdalah Juma. Mhe. Ndugai anatarajia kurejea
nchini kesho jumatano ambapo Bunge la Afrika linaendelea na Vikao vyake
hadi tarehe 13 Mei, 2016.
0 comments :
Post a Comment