Video:Dk Tulia Akomalia Kuitwa Muheshimiwa Bungeni....Silinde Agoma...


Msemaji wa Kambi ya Upinzani wa Wizara ya Fedha na Mipango, David Silinde, amejikuta kwenye mvutano na Naibu Spika, Dk Tulia Ackson, baada ya kuanza kusoma bajeti mbadala bila kumuita mheshimiwa naibu spika.

Silinde alianza kuwasilisha bila ya kumtaja Naibu Spika, Dk Tulia Ackson, hivyo kusababisha wabunge wa CCM kuguna.

Kutokana na miguno hiyo, Dk Tulia alimtaka akipe kiti heshima yake, lakini Silinde akamkatalia akisema si lazima kumwita Tulia mheshimiwa kabla ya kukubali kwa shingo upande.

“Kama unataka uheshimiwa sawa,” alisema Silinde na kuongeza: “Basi Mheshimwa Naibu Spika,” alisema na kusababisha ukumbi kupiga makofi.



Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment