MWANASHERIA WA TAKUKURU MBARONI KWA RUSHWA



MWANASHERIA wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) wa wilaya ya Makete mkoani Njombe na mlinzi wa ofisi za taasisi hiyo wilayani humo, wanashikiliwa na Takukuru wakituhumiwa kuomba na kupokea rushwa.

Watumishi hao wanaotuhumiwa kuomba rushwa ya Sh 600,000 kutoka kwa mtumishi anayetuhumiwa kughushi vyeti vilivyomuwezesha kupata ajira.

Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Njombe, Charles Nakembetwa alimtaja mwanasheria huyo kuwa ni Frednand Nsakuzi na Julius Hasani ambaye ni mlinzi wa ofisi ya taasisi hiyo.

Akizungumza na wanahabari ofisini kwake jana, Nakembetwa alisema watumishi hao waliomba rushwa kwa mtumishi huyo ili kuficha ukweli wa taarifa alizohusishwa nazo.

Alisema Takukuru kwa kushilikiana na mteja wao huyo waliweka mtego uliofanikisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao.

Alisema katika mtego uliotegwa Juni 28, mwaka huu, watuhumiwa hao walipokea Sh 100,000 kama malipo ya awali katika tukio lilifanyika kati ya saa moja na mbili usiku.

“Wakakamatwa wakati wakipokea kiasi hicho cha fedha kinyume na Kifungu cha 15 cha Sheria  ya Kuzuia na Kupambana Na Rushwa Namba 11  Ya Mwaka 2007,” alisema.

Huku uchunguzi ukiendelea, alisema watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani wakati wowote kuanzia sasa.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment