Kiongozi wa Taasisi na Jumuiya za Kiislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda 
amempongeza Rais John Magufuli kutokana na ahadi yake ya kurejesha mali 
za Waislamu. 
Lakini Sheikh Ponda hajakubaliana na kitendo cha Rais 
kutoa fedha taslimu kwa ajili ya kuchangia safari za Hija, akisema mkuu 
huyo wa nchi angezungumza na wahusika ili kujua matatizo ambayo fedha 
hizo zingesaidia. 
Sheikh Ponda amesema ahadi hiyo ya Rais ni ya kuungwa mkono kwa kuwa 
inaonyesha kujali masilahi ya wananchi, hususan Waislamu. 
Juzi, 
akihutubia Baraza la Idd el Fitr jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli 
alisema atawasaidia Waislamu kurejesha mali zao na kumpongeza Mufti wa 
Tanzania, Sheikh Mkuu, Abubakar Zubeir kuwa alikuwa mstari wa mbele 
katika kurejesha mali hizo kabla hata hajapewa cheo hicho. 
“Nakumbuka 
wakati nikiwa Waziri wa Ardhi, kabla hujawa Mufti, pamoja na viongozi wa
 Bakwata na wengine, ulifika ofisini kwangu ukieleza jinsi mali za 
Waislamu zilivyokuwa zinadhulumiwa. 
"Ninafamu pamekuwa na hiyo tabia ya 
baadhi ya viongozi wenye mali kuwatumia viongozi wa Bakwata na dini 
nyingine katika kuwarubuni na kuingia ubia. Mali hizo baadaye huwa 
zinapotea kabisa,” alisema. 
“Tujitahidi kwa nguvu zote kusimamia mali 
hizi zisije kuwa chanzo cha kuvunjika kwa amani. Tunapenda wawekezaji, 
lakini wanachokiahidi hawatekelezi. Haiwezekani. 
“Haiwezekani na wala 
haikubaliki kwa watu kwa ujanja wao na wakati mwingine kwa kutumia 
wanasheria wao kukalia mali za Waislamu. Mali za Waislamu lazima zirudi 
na za Wakristo zirudi ili amani iwepo.” 
Sheikh Ponda alisema kwa kauli 
hiyo, Rais Magufuli ametambua juhudi ambayo wamekuwa wakizifanya katika 
kupigania mali za Waislamu, kama ilivyokuwa katika kupigania kiwanja cha
 Chang’ombe hadi kusababisha kesi dhidi yake na wenzake. 
“Utakumbuka, 
tulikuwa na kesi kuhusu kiwanja cha Waislamu kule Chang’ombe, katika 
hatua za awali tulishindwa, lakini baadaye tukakata rufaa na kushinda. Ndiyo sababu ya kuunga mkono kauli hii ya Rais,” alisema Sheikh Ponda. 
Akizungumzia msaada wa Rais Magufuli kwa ajili ya Hija, alisema hiyo ni 
ruzuku muhimu, lakini Rais angekaa na Waislamu wamweleze mambo ambayo ni
 muhimu zaidi ili uwekezaji wake uwe na manufaa zaidi. 
Alipoulizwa ni 
mambo gani ni muhimu zaidi, Sheikh Ponda alisema ni masuala ya elimu na 
afya ambayo Serikali ikisaidia baadaye yatapunguza mzigo mkubwa kwake



Blogger Comment
Facebook Comment