Serikali
kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), jana imezifungua ofisi za
Kampuni maarufu ya uwakili ya Mbunge wa Butiama, Nimrod Mkono, ikiwa ni
siku chache baada ya kuzifungia kwa madai kuwa kampuni hiyo inadaiwa
kodi ya shilingi bilioni 1.
TRA
waliwasili katika jengo la ofisi hizo zilizoko katika jengo la Bank ya
Exim iliyoko jijini Dar es Salaam (ingawa ilikuwa sikukuu), pamoja na
Kampuni ya udalali ya Yono na kuzifungua ofisi hizo mbele ya Nimrod
Mkono na binti yake.
Mkurugenzi
wa huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo amekiri
kufunguliwa kwa ofisi hizo. Kayombo amesema kuwa uamuzi huo ulifikiwa
baada ya kuwepo kwa makubaliano kati ya pande mbili na ahadi ya kufanya
malipo iliyowekwa na mkono.
“Ni
kweli muda upo tuliokubaliana lakini hatutaki uwe katika vyombo vya
habari, kutokana na nia ya dhati aliyoonesha Mkono ndio maana
tumekubaliana nae,” Kayombo anakaririwa.
Hatua
hiyo imefikiwa huku kukiwa na taarifa kuwa ingawa Mkono amefungiwa
ofisi zake akidaiwa kodi ya shilingi bilioni 1, yeye anaidai Serikali
takribani shilingi bilioni 9 kwa kazi alizofanya ndani ya Tanzania Bara
na Zanzibar.



Blogger Comment
Facebook Comment