Licha ya kuwa kipenzi cha kocha wa Arsenal, Arsene Wenger pamoja na mashabiki wa klabu hiyo lakini hali inaonekana kuwa tofauti kwa kiungo Jack Wilshere kwa kuwa na hatihati za kukosekana kwa msimu wa 2016/2017.
Hatua hiyo inakuja baada ya kocha wa Arsenal, Wenger kuwa tayari kumtoa kiungo huyo kwa mkopo katika klabu nyingine ili aweze kujijenga upya na kurudi katika makali yake baada ya kuwa akisumbuliwa na majeruhi mara kwa mara.
Kwa sasa Arsenal inaonekana kuwa na kikosi kipana zaidi wachezaji ambao wanacheza nafasi moja na Wilshere, ambapo wachezaji hao ni pamoja na Santi Cazorla, Granit Xhaka, Aaron Ramsey, Francis Coquelin na Mohamed Elneny.
Aidha pamoja na uamuzi huo wa kocha Wenger kumtoa kwa mkopo Wilshere ameonekana kuwa mgumu kumtoa kwa vilabu ambavyo vinagombania nafasi nne za juu katika Ligi Kuu ya Uingereza ambazo ni pamoja na Manchester City, Manchester United, Tottenham na Liverpool.
Welshere mpaka sasa ameichezea Arsenal dakika 37 pekee katika michezo ya maandalizi na ndani ya masaa 24 yajayo anatarajiwa kuwa tayari amepata timu ya kujiunga kwa mkopo.